Siku ya leo macho na masikio ya watanzania hasa wafuasi na wapenzi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA) yalielekezwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, pale ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Jaji John Utumwa alikuwa akitoa hukumu dhidi ya kesi ya Zitto Kabwe na uongozi wa juu wa CHADEMA.
Zitto ambaye alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, alifungua kesi katika Mahakama hiyo akipinga hatua ya Kamati Kuu ya Chama hicho iliyokutana tarehe 3 na 4 mwezi huu kujadili hatima ya uanachama wake wakati baraza kuu halijakaa na kujadili rufaa yake ya kupinga kuvuliwa nyadhifa zake zote za uongozi ndani ya chama hicho...
Akisoma hukumu ya kesi hiyo baada ya kuiahirisha jana, Jaji wa mahakama hiyo,Jaji Utamwa ameridhia pingamizi lililotolewa na mh. Zitto Kabwe la kutojadili uanachama wake na kuitaka kamati kuu ya CHADEMA au chombo kingine chochote kisijadili uanachama wake hadi kesi yake ya msingi ( rufaa ) itakaposikilizwa na baraza kuu la chama hicho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.