Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho a.k.a Injili,na anaetamba na wimbo mpya wa Facebook, Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya jana ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati wa muendelezo wa tamasha la Krisimasi lililofanyika leo Mkoani Tanga. Tamasha hilo ndio kwa mara ya kwanza linafanyika mkoani humo, limezindundiliwa jijini Dar siku ya Krisimasi ndani ya uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na watazamaji lukuki. Tamasha hilo baada ya kufanyika mkoani Tanga, kesho litafanyika jijini Arusha na baadae mkoani Dodoma likiwajumuisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili. |
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.