ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 12, 2013

MATEKE KUPIGWA PAMBANO LA KASEBA

MATEKE  KUPIGWA  PAMBANO  LA  KASEBA


Lile pambano linalosubiriwa kwa hamu kubwa kati ya  bondia Alibaba Ramadhan na bingwa Japhet Kaseba litakuwa na sura nyingine ya mapigano kwa muandaaji wa pambano hilo Ibrahim Kamwe kuongeza mapambano  ya  kick boxing (ngumi na mateke) ili kuleta radha zaidi.
Hayo yamejitokeza baada ya bondia mtanzania anayeishi nchini Canada Kareem Kutch akiwa kama raia wa huko kutokana na wazazi wake kuwa wakanada kuripoti kuwa Tanzania hakuna wachezaji wa kiwango cha kimataifa na hakuna  mtu wa kucheza na yeye  jambo ambalo lilipingwa na mabondia wa hapa nchini.
Kwa kuona hivyo Bigright Promotion, ikamtafuta mtu anayemfaa kukanusa kauli hiyo na hatimaye imefanikiwa kumpata bondia  `Tata boy` ambae amekubali kucheza nae katika uzani wa kilogram 75 za mchezo wa kimataifa.
Ni katika pambano litakalopigwa siku hiyo ya jumapili ya tareha 22 decemba katika ukumbi wa Friends Corner Hotel, siku ambayo kutakuwepo na mapambano mengi yakiwemo ya Enerst Bujiku kuzipiga na Sha Kasim, Lusekelo Daud dhidi ya Mbaruku Kheri, Issa Omar atapigana na Haji Juma, Moro Best na Isa Peche.
Aidha kutakuwa na mapambano mengi ambapo kwa ufupi yamepangwa kuwa mapambano ya kuikaribisha  X-mass na Mwaka mpya kwa staili ya aina yake na kuuaga mwaka 2013 kwa usalama na amani.
Mapambano hayo yatasimamiwa na PST chini ya kiongozi wake Emanuel Mlundwa

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.