ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 10, 2013

HEBU SOMA WARAKA HUU WA TUNDU LISSU KWA WANAMABADILIKO.

Wanamabadiliko,
Nina mambo mawili. Moja, kwa kadri mjadala huu ulivyo hadi sasa, inaelekea kuwa kila mmoja wetu anaamini kwamba ni kweli huyu bwana kafanyiwa fujo Kama anavyodai. Hii assumption kwamba anachosema kweli kimetokea haina msingi wowote zaidi ya maneno yake mwenyewe. Hajatoa ushahidi wowote kuthibitisha madai yake. Hajataja jina la Mhusika hata mmoja aliyeshiriki kumfanyia fujo. Mwanasheria wa BAVICHA could be me, I was there na nadhani huyu bwana ananifahamu, Kama sio kwa jina angalau kwa sura. Ameulizwa Kama ametoa taarifa polisi, inaelekea hajatoa. Lakini hata Kama angekuwa ametoa would it necessarily be true kwamba amefanyiwa fujo? Si itakuwa ni tuhuma tu zinazohitaji uthibitisho? Kinachonisumbua ni hicho kwamba badala ya kumhoji juu ya ukweli wa maneno yake tunayajadili as if yamethibitishwa kwamba ni ya kweli.

Pili, it seems to me hadithi hii, pamoja na mapungufu yake mengi, ina lengo moja tu: kuichafua na kuipaka matope CHADEMA. Choice ya kichwa cha habari 'NIMEFANYIWA FUJO KONGAMANO LA UHURU CHADEMA' ni ya makusudi na ina lengo hilo. Swali kama waliomfanyia fujo, kama ni kweli, wametumwa na viongozi au la ni la makusudi na lengo ni hilo hilo. 

Tatu, kama nadharia yangu ni ya kweli kwamba hadithi hii lengo ni kuichafua CHADEMA na viongozi wake, then haitakiwi kutustaajabisha hata kidogo. Huu ni mwendelezo wa vita ya ugaidi dhidi ya Wilfred Lwakatare, Henry Kilewo na wenzao na CHADEMA iliyoanza mwaka jana na kuisha katikati ya mwaka huu Mahakama Kuu Dar na Tabora. Mshiriki Mkuu (MM?) wa vita hii alikuwa Mwigulu Nchemba, Dennis Msaki, MM mwingine wa majuzi na mapolisi akina Advocate Nyombi na kundi lao!

Kwa wasiokumbuka naomba nirudie kilichotokea. Kwa zaidi ya mwezi mzima kabla ya tarehe 28 Desemba, Ludovick alikuwa akiwasiliana na Dennis Msaki kwa simu kuliko alivyokuwa akiwasiliana na mke wake wa ndoa. Siku ya tarehe 28 Desemba (wakati au kabla au baada ya kumrekodi Lwakatare kwa Siri) aliwasiliana kwa simu na Mwigulu Nchemba. Kesho yake tarehe 29 asubuhi Mwigulu Nchemba, MM na Julius Mtatiro wa CUF walionekana kwenye Star TV ambapo Mwigulu Nchemba alidai kuwa na ushahidi wa video wa viongozi wa CHADEMA wakipanga mauaji ya waandishi habari. MM hakumkanusha! Tarehe 14 Januari 2013 Mwigulu Nchemba alimtumia Ludovick sh. 50,000 kwa M-Pesa.

Baadae video ya ugaidi wa CHADEMA ilipowekwa kwenye YouTube na Lwakatare kukamatwa, MM alikuwa kiongozi pekee wa CHADEMA aliyeandika kwenye mtandao hadharani kwamba Lwakatare asimamishwe uongozi ili achunguzwe kuhusiana na njama hizi za kigaidi. The message was loud and clear: CHADEMA should distance itself from it's security chief ili anyung'unywe peke yake bila msaada halafu akipatikana na hatia, iwe ni hatia ya chama pia! Ni bahati mbaya tu kwamba mipango hii ilishindwa baada ya chama hiki chenye watu wenye 'akili ndogo' na 'elimu ya magumashi' walidaka ushahidi wote huu na kupambana na wajanja na wasomi hawa hadharani!

Ludovick na wanaomtumia walishindwa Mara ya kwanza. Wanafikiri watashinda Mara ya pili. Tusubiri!

Tundu

CHANZO:-mabadilikotanzania@googlegroups.com

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.