Airtel yamwaga zawadi ya milioni 40 katika 'Mimi ni Bingwa' promosheni
Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzani imeshazawadia wateja wake zaidi ya shilingi milioni 40 katika promosheni yake ya 'Mimi ni Bingwa' yenye lengo la kuwazawadia wateja wake na kuongeza chachu ya mpira wa miguu nchini.
Hii ilithibitishwa na Meneja Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando wakati wa kuangalia mechi ya Ligi kuu ya Uingereza kati ya klabu ya Manchester United na Newcastle iliyoonyeshwa bure eneo la Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam.
Alisema mbali na zawadi ya fedha inayotolewa kwa kutumwa kupitia Airtel Money, washindi wawili wa tiketi pamoja na safari inayogharamiwa na Airtel kwenda kuangalia mechi moja kwa moja (live) za klabu ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford, watasaidiwa katika utafutaji wa hati za kusafiria pamoja na washindi wawili watakaopatikana katika droo ya wiki ya tatu na nne.
Mmbando ambae wakati wa tukio pia alitangaza washindi wengine watano wa shilingi milioni moja kila mmoja wa wiki hii, alisema promosheni inayotokana na ushirikiano kati ya Manchester United na kampuni hiyo ya simu hailengi tu kuwazawadia wateja lakini pia kuwaunganisha wateja na soka la kimataifa hatua ambayo itaongeza chachu ya wapenda michezo Tanzania.
''Airtel imeweka vituo mbali mbali ambavyo wapenda soka wataangalia mechi za klabu ya Manchester United bure kupitia luninga kubwa. Leo tunawaonyesha wakazi wa Mbagala mechi kati ya Manchester United na Newcastle, lakini pia tunavituo vingine ambavyo tunaonyesha mechi zote za Man U bure. Vituo hivi ni kama Mbeya, Shaba Pub Mwanza -Shooters Pub, Dodoma - Four Ways, Dar es Salaam - Rose Garden, Morogoro - Nyumbani Launge na Arusha - Empire Sports bar,'' alisema Mmbando.
Mmbando alisema kuwa bado zawadi nyingi kushindaniwa na kusema kuwa mbali na shilingi milioni 2 za kila siku, milioni 10 kila wiki na tiketi 2 kwa watu wawili kila wiki, bado kuna zawadi ya kubwa ya shilingi milioni 50 kushindaniwa mwishoni mwa promosheni.
Alisema ili mteja kushiriki kwenye promosheni, anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) yenye neno "BINGWA" kwenda namba 15656.
Licha ya washabiki wa Man U kuvunjika moyo baada ya kufungwa goli moja na Klabu ya Newcastle United katika mechi iliyochezwa uwanja wa Old Trafford waliburudishwa na wasanii wa Bongo Flava kama Ney wa Mitego, Young Killer na Kinoko Comedy Group.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.