ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 25, 2013

MH. LOWASSA AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KATA YA SARANGA,KIMARA JIJINI DAR

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiburudika kwa kucheza muziki sambamba na wakina Mama wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam,Mwishoni mwa wiki wakati alipokwenda kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo.Zaidi ya Sh. Mil. 100 ziliweza kupatikana kwenye harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipena mikono na Wakazi mbali mbali wa Kata ya Saranga,Kimara wakati akiendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisisitija jambo kwa wananchi wakazi wa Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya pili ya Sekondari katika Kata hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Diwani wa Kata ya Saranga (CHADEMA),Mh. Ephraim Kinyafu akizungumza machache wakati wa harambee hilo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Kata ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa NEC (CCM) Wilaya ya Kinondoni,Kalist Lyimo akisisiza jambo kwa wakazi wa Saranga,Juu ya umuhimu wa kuchangia harambee hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Saranga,Gwelino Kalinga akizungumza wakati wa Ufunguzi wa harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipena mkono na Mjumbe wa NEC (CCM) Wilaya ya Kinondoni,Kalist Lyimo.
Mmoja wa wakazi wa Kata hiyo ya Saranga akizungumza.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapongeza vijana wa Chipukizi mara baada ya kutoa ngonjera nzuri.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiangalia burudani iliyokuwa ikitolewa na wakazi wa Kata ya Saranga.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimsikiliza kwa makini Diwani wa Kata ya Saranga (CHADEMA),Mh. Ephraim Kinyafu wakati akimueleza jambo.
Sehemu ya wakazi wa Kata hiyo ya Saranga,Kimara jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye hafla hiyo ya Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya kata hiyo.Picha Zote na Othman Michuzi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.