AIRTEL SHULE YETU YAFAGILIWA NA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ILULU -LINDI ,
Airtel Marketing Manager of the Southern zone and Morogoro region Aminata Keita instructing students of Nanyamba Secondary school in Mtwara on how to use books soon after handing over text books worth 5/- m to the school donated by Airtel Tanzania.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Ilulu iliyoko wilayani Kilwa mkoani Lindi,wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuwapatia msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni tano.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Ilulu iliyoko wilayani Kilwa mkoani Lindi,wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuwapatia msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni tano.
Wakizungumza shuleni hapo mara baada ya kupokea msaada huo wanafunzi hao wamesema kwamba wanafunzi wasichana wanauwezo wa kusoma masomo ya sayansi na kufanya vizuri isipokuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa maabara na vitabu.
Wanafunzi hao wameishukuru kampuni ya simu ya airtel na kusema kwamba hivi sasa watasoma kwa bidii masomo hayo ya sayansi kwani kukosekana kwa vitabu hivyo kulikuwa kunachangia kutofanya vizuri katika masomo hayo.
"Tumekua tunapata shida sana kujifunza masomo ya sayansi kwani hapa shuleni kwetu hakuna hata maktaba wala maabara kwa ajili ya masomo hayo," alisema Rehema Issa.
"Vitabu hivi vitatuwezesha kufaulu masomo yetu ya sayansi japo bado tunakabiwa na tatizo na maabara aliongeza Blandina Charles mwanafunzi wa kidato cha tatu shuleni hapo.
Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa morogoro Aminata Keita, amesema msaada huo ni mchango wa airtel katika elimu hapa nchini.
Keita amesema zoezi hilo la kutoa vitabu vya masomo ya sayansi linaendelea katika shule 35 za sekondari hapa nchini ili kuwawezesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.
"Kwetu sisi Airtel hii ni fahari kubwa kushirikiana na shule hii katika kukuza ufaulu hasa kupitia vitabu hivi vya kiada ambavyo ni vya masomo ya sayansi" alisisitiza Keita.
"Mpaka sasa tumezifikia shule nyingi sana na Ilulu secondary imepata fursa ya kupata msaa huu, nawasihi mvitumie vitabu hivi kwa manufaa yenu na wenzenu watakaosoma hapa," alimalizia Aminata
Utaratibu wa kusaidia elimu kupitia mpango wa shule yetu ulio chini ya kampuni ya simu za mkononi ya airtel unachangia ukuaji wa sekta ya elimu kupitia vitabu vya masomo ya sayansi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.