Renatus Luneja. |
BODI ya Pamba nchini kupitia Mfuko wake wa Maendeleo (EDF) kutumia kiasi cha zaidi shilingi milioni 800 kujenga Maghala 28 mapya na kukarabati mengine 20 ya Vyama vya Msingi ili kuhifadhia Pamba Katika Wilaya za Maswa, Meatu, Bariadi na Itilima Mkoani Simiyu.
Luneja alifafanua
kuwa kutokana na wakulima na vikundi vya wakulima kutumia kuhifadhi pamba yao
katika maghala hayo wakisubilia ununuzi au kuhifadhiwa ndani ya maghala hayo
baada ya kununuliwa na kuharibika imekuwa ikizua malalamiko ya mara kwa mara
kuhusu Ubora wa Pamba ya Tanzania kwenye Soko la ndani na Dunia na kusababisha
kuwa na bei punguzo.
Mratibu wa Mradi huo unaofadhiliwa kwa miaka mitatu na Jumuiya ya Ulaya (EU), Renatus Luneja alisema kwamba lengo ni kuongeza usafi wa pamba na kudhibiti uchafuzi ambao umeonekana kuwa changamoto wa kurudisha juhudi za zao hilo kuwa na thamani ya Pamba Dhahabu Nyeupe ili kuwa na soko la uhakika ndani nan je ya nchi.
Luneja alisema kwamba kutokana na Maghala mengi kuwa na hali ambayo haikidhi kuifadhi pamba kwa ubora unaotakiwa kabla ya kupelekwa viwandani kuchambuliwa katika maeneo mbalimbali vya Vyama vya Msingi vijijini ilipelekea Jumuiya ya Ulaya kuamua kutoa fedha za kukarabati na kujenga maghala hayo kabla ya kuanza kwa Msimu wa mwaka 2013/2014.
“Mengi ya Maghala haya yamejengwa miaka ya 1960 hadi 1970 hivyo kuonekana kuchakaa na kutokuwa tena na hadhi ya kuhifadhi pamba kwa ubora unaotakiwa na hivyo kuchangia kwa kiasi katika uchafuzi wa pamba inayokuwa imehifadhiwa baada ya kununuliwa kutoka kwa wakulima vijijini” alisema
Mratibu huyo alisema kwamba baada ya kutembelea Wilaya za Maswa, Meatu na Bariadi na kujionea maghala hayo ambayo mengi yanaonekana kuvuja, kuoza mabati na hata kuanguka kutokana na kutofanyiwa ukarabati kwa miaka mingi tangu yalipojengwa na Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) huchangia uchafuzi wa pamba” alisisitizaMaghala haya yamejengwa miaka ya 1960 hadi 1970 kwa mifumo ya kizamani isiyokidhi hali ya sasa yenye changamoto nyingi. |
Kwa maghala kama haya hakuna haja ya kuuliza kwanini hatupati pamba safi. |
Mratibu huyo
alieleza kuwa mradi huo unataraji kukamilika ifikapo mwezi wa April mwaka 2014
kabla ya kuanza kwa msimu wa ununuzi wa pamba ambapo kwa sasa tathimini ya
kubaini maeneo na kuomba maeneo kutoka kwa serikali za vijiji imefanika huku
kikwazo kikionekana kuwa kwa maafisa ardhi kutoyatambua na kuyapima kasha kutoa
Hati Miliki kwa vijiji.
Kwa Upande wake
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Erasto Sima ametoa Wito kwa wakulima wawezeshaji na maafisa ugani wa Kata na Tarafa kuwaelimisha
wakulima kwa kufuata kanuni bora za kilimo cha zao la pamba ikiwemo kulidhia
kilimo cha Mkataba na wawekezaji ili kujikwamua na ndicho kilimo pekee chenye
tija kwa wakulima ili kuwapatia kipato na kuboresha maisha ya familia zao
ikizingatiwa kuwa asilimia 80 hutegemea ajira ya kilimo kwa wananchi wengi wa
vijijini
Mkuu huyo pia
aliwataka wakulima na vikundi vya wakulima wa zao la pamba kuwa makini kuingia
Mkataba na wawekezaji ili kutokuwepo malalamiko wakati wa msimu wa kuuza pamba
yao huku pia akiwataka wawekezaji kupeleka pembejeo mapema kabla ya msimu wa
kilimo kuanza na kufunga mikataba kwa wakati ili kuwa na uhakika kwa wakulima
na vikundi kuanza kilimo kwa wakati.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.