ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 30, 2013

WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI KIRUMBA WARAHISISHIWA BIASHARA NA AIRTEL MONEY

Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mbando (kushoto) akinunua samaki kwa njia ya Airtel Money toka kwa moja kati ya wachuuzi  katika Soko la Kimataifa la samaki Mwaloni Kirumba jijini Mwanza, ambapo Airtel ilifika sokoni hapo kujionea jinsi wafanyabiashara hao wanavyoitumia huduma yao ya kutuma na kutoa pesa bila makato. Hakatwi mtu hapa.
Rashidi Moshi ni moja kati ya wavuvi na wauzaji samaki katika Soko la Kimataifa Mwaloni Kirumba jijini Mwanza na hapa alikuwa akitoa maelekezo juu ya moja ya bidhaa hizo za samaki aina ya Sangara wanaounzwa nje ya nchi na kuwapatia riziki kujikwamua kimaisha.
"Samaki huyu hunaswa na ndoano hii ndogo tu ambayo ikimkamata hafurukuti babaake" Ndivyo alivyokuwa akisema Rashid kwa wadau hao wa Huduma za mawasiliano ya simu za mkononi (Airtel), ambapo Airtel ilifika sokoni hapo kujionea jinsi wafanyabiashara hao wanavyoitumia huduma yao ya kutuma na kutoa pesa bila makato. Hakatwi mtu hapa.
"Sasa ndoano hii humnasa hapa"
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mbando (kulia) akichagua samaki toka kwenye meza ya Bw. Isaac Simon ambaye mbali na kuuza kwa njia ya fedha taslimu pia huitumia huduma ya Airtel Money katika malipo  katika Soko la Kimataifa la samaki Mwaloni Kirumba jijini Mwanza. Airtel ilifika sokoni hapo kujionea jinsi wafanyabiashara hao wanavyoitumia huduma yao ya kutuma na kutoa pesa bila makato. Hakatwi mtu hapa.
Mpangilio mzuri wa samaki walio kaushwa aina ya Sangara tayari kwa biashara.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mbando (kushoto) akiwa na Afisa Masoko wa Airtel mkoa wa Mwanza Ally Mashauri  wakimkabidhi vitendea kazi Bw. Innocent Godwin anayefanya Uwakala eneo la Soko la Kimataifa la samaki Mwaloni Kirumba jijini Mwanza, ambapo Airtel ilifika sokoni hapo kujionea jinsi wafanyabiashara wanavyoitumia huduma yao ya kutuma na kutoa pesa bila makato. Hakatwi mtu hapa.
Mwananchi huyooooo.... 'akisepa' na kitoweo chake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.