Na: william severine/mathias haule/grace george(Wanafunzi DACICO).
Wanafunzi wa Chuo cha Dar es Salaam City College kilichopo jijini dar es salaam manispaa ya kinondoni, leo wamefanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wao katika nafasi ya urais na makamu wa rais kutokana na uongozi uliopo madarakani kumaliza muda wao ,
Wakizungumzia tukio hilo kwa nyakati tofauti,baadhi ya wanafunzi walisema kuwa tukio hilo limechukua muda mrefu sana kufikia uchaguzi huo kutokana na kuairishwa kwa tarehe ya mwanzo ambayo ulipangwa kufanyika October 22 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume ya kamati ya kusimamia Uchaguzi huo Mussa Moses alisema kuwa sababu za kusogezwa mbele ni kutokana na tume kutokuwa makini na kile kilichoelezwa kuwa ni kuruhusu uongozi wa juu wa chuo kuingilia maamuzi yao kama tume ya uchaguzi.
Hata hivyo mwenyekiti wa tume hiyo ya uchaguzi ndugu musa moses alipinga tuhuma hizo na kusema kuwa tume haikuingiliwa katika maamuzi yake bali walikubali maombi yaliyo toka uongozi wa juu wa chuo ya kuomba kuuboresha uchaguzi huo na kuomba ufanyika October 30 mwaka huu.
Pia mmoja wa wagombea hao katika nafasi ya urais ndugu, Mathias Canal alisema anashukuru hatua ambayo chuo kimefikia cha kufanya uchaguzi huru na kutoa pongezi zake kwa tume ya uchaguzi kwa kufanikisha zoezi hilo.
Wagombea waliojitokeza katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Mathias Canal,Hilary Mgenzi,Christopher Mwakasanga(Urais) na kwa nafasi ya Makamu wa Urais ni pamoja na Razack Mushi, Mathias Haule, na Rozalina Mchomvu.
Aidha mkurugenzi wa chuo mr. idrisa mziray alitoa pongezi kwa wanafunzi wote kwa kujitokeza na kushiriki katika tukio hilo la upigaji kura kutoka na kuwa ni haki yao ya kimsingi ili kujipatia viongozi walio bora kwa maslai yao na chuo kwa ujumla.
"Uchaguzi Umekwenda Vizuri, kikubwa nawapongeza wanafunzi wote kwanza kwa kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura, pia nawapongeza wasimamizi kwa kuandaa Uchaguzi huru na wa haki maana wametimiza misingi ya Demokrasia, hakuna malalamiko kutoka pande zote, hili ni jambo la kujivunia sana, kwa kuwa chaguzi nyingi vyuoni uambatana na vurugu na pia Rushwa za hapa na pale" alisema Mziray
Matokeo ya Uchaguzi huo yanatazamiwa kutangazwa mapema kesho baada ya kuhesabiwa na wasimamizi wa Tume ya Uchaguzi huo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.