ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 23, 2013

TOP LAND KINONDONI MABINGWA SAFARI POOL 2013.

Naibu Waziri wa Utamaduni,Vijana na Michezo, Amos Makala(wa tatu kulia) akimkabidhi kikombe nahodha wa klabu ya Topland ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni,Omari Akida mara baada ya kuibuka mabi ngwa katika fainali za kitaifa za mashindano ya Safari National Pool yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Mweka hazina wa chama cha Pool Taifa (TAPA), Zaholo Ligalu.

TOP LAND KINONDONI MABINGWA SAFARI POOL 2013.
Na Mwandishi Wetu.Morogoro.
KLABU ya Top Land kutoka mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za mashindano ya Safari Pool 2013, yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.

Top land walitwaa ubingwa huo kwa kuifunga klabu ya Mpo Afrika ya Temeke 13-10 na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 5,000,000/=, Kikombe na medali za Dhahabu kwa kila mchezaji.

Mshindi wa pili katika fainali hizo ni klabu ya  Mpo Afrika ambayo ilizawadiwa fedha taslimu shilingi 2,500,,00/= na Medali za Fedha kwa kila mchezaji.

Mshindi wa tatu  ni klabu ya Supersport kutoka mkoa wa Manyala ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 1,250,000/= na medali za shaba na mshindi wan ne ni klabu ya Mashujaa kutoka mkoa wa kimichezo wa Ilala ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 1,000,000/=

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(singles), mchezaji Festo Yohana kutoka klabu ya Mashujaa ya mkoa wa kimichezo wa Ilala alitwaa ubingwa wa Taifa kwa kumfunga Mussa Mkwega kutoka Morogoro 5-1 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000/=,Kikombe na medali ya dhahabu ambapo mshindi wa pili ulichukuliwa na Mussa Mkwega ambaye alijinyakulia fedha taslimu shilingi 350,000/= na medali  ya Fedha.

Mshindi wa tatu ni Mohamed Idd kutoka klabu ya Atlantic ya mkoani Dodoma ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000/= na medali ya shaba ambapo mshindi wa nne ni Ernest John kutoka Tabora ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/=.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanawake(Singles), mchezaji Rose Deus kutoka mkoa wa Morogoro alitwaa ubingwa wa kitaifa kwa kumfunga Cecilia Kileo kutoka Ilala 5-4 na hivyo Rose kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000/= Kikombe na medali ya Dhahabu ambapo Cecilia alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000/=na medali ya Fedha.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na mchezaji Merry Gumbu kutoka Arusha ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/= na medali ya shaba na nafasi ya nne ilichukuliwa na Judith Machafuko kutoka mkoa wa Kinondoni ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 100,000/=.

Fainali hizo za kitaifa zilihudhuliwa na Naibu Waziri wa Utamaduni,Vijana na Michezo, Amos Makala  ambaye alikipongeza chama cha Pool Taifa(TAPA) kwa kuufikisha mchezo hapo ulipo ambapo mpaka sasa umesambaa katika mikoa 17 ambayo ilishiriki mashindano hayo na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kama serikali kwa kuutambua na kutoa mchaada watakapohitaji.

Makala pia aliipongeza TBL kupitia Bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mchezo wa Pool kwa mwaka wa sita sasa na kuwaomba waendelee kudhamini kwa miaka ijayo.Lakini pia alimpongeza Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo kwa Brand yake ya Safari kuwa bia namba moja Afrika na kumuomba aendelee kudhamini Pool ikamate namba moja katika mashindano ya Pool ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Malawi hivi karibuni.

Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo alikipongeza chama cha Pool kwa kumaliza fainali salama na kuahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo, lakini pia aliwapongeza Mkoa wa Pwani ambao mwaka huu ni mra yao ya kwanza kushiriki fainali hizo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.