ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 23, 2013

NCHIMBI AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI JIJINI MWANZA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi akihutubia wananchi wa mkoa wa Mwanza walio hudhuria Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani inayofanyika kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Kushoto ni mwenyeji wa maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo na wengine kutoka kulia ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani nchini Kamanda Mpinga akifuatiwa na Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Pereila Sirima.
Maandamano ya Maadhimisho haya ya Wiki ya Usalama Barabarani yakiwa katika barabara ya Makongoro jijini Mwanza.
Wadau wa chama cha waendesha vyombo vya moto barabarani wakiwa na bango lao lenye ujumbe.
Wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Mwanza wameshiriki Maadhimisho haya ya Wiki ya Usalama Barabarani wakiwa kama moja ya sehemu ya wadau watumiao barabara wakihitaji elimu kwa matumizisahihi ya barabara kuepusha ajali.
Wadau mbalimbali kutoka sekta za usafirishaji, madereva wa boda boda, madereva wa taxi na askari wa vikosi vya usalama barabarani mkoa wa Mwanza, wameshiriki Maadhimisho haya ya Wiki ya Usalama Barabarani wakiwa kama moja ya sehemu ya wadau watumiao barabara wakihitaji elimu kwa matumizisahihi ya barabara kuepusha ajali.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwandishi wa Habari Athumani Hamisi ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Usalama Barabarani, mwandishi huyu alipata ajali ya gari ambayo ilisababisha baadhi ya viungo vyake kupooza licha ya kupata matibabu nchini Afrika ya Kusini na India.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Airtel Tanzania ambao wamekuwa wadhamini wakuu wa Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kwa mwaka wa tatu mfululizo Bi. Beatrice Singano Mallya akisalimiana na  Mwandishi wa Habari Athumani Hamisi ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa Usalama Barabarani. Athumani alipata ajali ya gari ambayo ilisababisha baadhi ya viungo vyake kupooza licha ya kupata matibabu nchini Afrika ya Kusini na India.
Wadau wa Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi Airtel Tanzania wakiwa wamejumuika na wadau wa makampuni menginge katika picha ya pamoja na mwanahabari Athumani Hamisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Emmanuel Nchimbi akizungumza ndani ya banda la Zimamoto mara baada ya kutinga mavazi ya kitengo hicho.




PIX 7 fd589
Picha ya pamoja Kwa maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani ambapo kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni "USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE". 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.