IRINGA
,MBEYA NA DODOMA WAPATA MABINGWA WA SAFARI POOL NGAZI YA MIKOA.
Na
Mwandishi Wetu.
MIKOA
ya Iringa, Mbeya na Dodoma hatimaye
imehitimisha fainali za mashindano ya Safari Pool Taifa ngazi ya mikoa na
kupata mabingwa wataowakilisha mikoa hiyo kwenye fainali za kitaifa
zinazotarajiwa kufanyika mkoani Morogoro.
Mkoa
wa Iringa upande wa timu,klabu ya Garden
ilifanikiwa kutwaa ubingwa kwa kuifunga klabu ya Ngija Masters 13-9 hivyo
kuzawadiwa kitita cha fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya
kuwakilisha mkoa wa Iringa kwenye fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Upande
wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Goodlover Ntalande kutoka klabu ya
Garden alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa kwa kumfunga Emmanuel Joseph 5-2,na
hivyo kujinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na
kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Upande
wa mchezaji mmoja mmoja wanawake, Naomi Ngede kutoka klabu ya Garden alitwaa
ubingwa kwa kumfunga Anna Elly 3-1, na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi
250,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Iringa kwenye fainali za
kitaifa mkoani Morogoro.
Mkoa
wa Dodoma,klabu ya Atlantic
ilifanikiwa kutwaa ubingwa hivyo
kwa kuifunga klabu ya Frolida na hivyo kuzawadiwa kitita cha fedha taslimu
shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Dodoma kwenye fainali za kitaifa mkoani
Morogoro.
Upande
wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Mohamed Idd alifanikiwa kutwaa
ubingwa wa mkoa kwa kumfunga Ramadhani Issa,na hivyo kujinyakulia zawadi ya
fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za
kitaifa mkoani Morogoro.
Upande
wa mchezaji mmoja mmoja wanawake, Zainabu Salum alitwaa ubingwa kwa kumfunga
Monica Siimule, na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 250,000/= pamoja na tiketi
ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Mkoa
wa Mbeya,klabu ya Royal
Zambezi ilifanikiwa kutwaa ubingwa kwa kuifunga klabu ya Shooters 13-2,na hivyo kuzwadiwa kitita cha fedha
taslimu shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa wa Mbeya kwenye
fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Upande
wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(Singles), Daniel Mbaga kutoka klabu ya Royal
class alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa kwa kumfunga Gibson Godwin 4-2,na
hivyo kujinyakulia zawadi ya fedha taslimu shilingi 350,000/= pamoja na
kuwakilisha mkoa wa Mbeya katika fainali za kitaifa mkoani Morogoro.
Upande
wa mchezaji mmoja mmoja wanawake, Rachel Richard kutoka klabu ya Kontena
Tunduma alitwaa ubingwa kwa kumfunga bingwa wa mwaka jana, Betty Sanga 3-2, na
kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 250,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha
mkoa kwenye fainali za
kitaifa mkoani Morogoro.
Akizungumza
na wachezaji pamoja na wakazi wa Mbeya,Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar
Shelukindo aliipongeza mikoa yote 17, kwa kumaliza vyema fainali za mashindano
hayo ngazi ya mikoa na hivyo kuviomba vilabu kujiaandaa kwa kwa muda uliobaki
kwa fainali ya kitaifa.
Shelukindo
aliisisitiza nidhamu katika mchezo ndio siri ya kila kitu katika mafanikio
mbele ya safari huko wanakoelekea kwenye fainali za kitaifa.Vilabu 17 kutoka
mikoa 17 vinatarajia kuchuana mkoani Morogoro na mwisho tutapata bingwa wa
Safari National Pool Championship 2013.
Fainali
za kitaifa zinatarajiwa kufanyika katika Mkoa wa Morogoro kuanzia Septemba 19
hadi 23,mwaka huu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.