Afisa Ubora wa Bia kutoka TBL Mwanza Jeremia Kamambi ndiye aliyekuwa mwenyeji wa Madiwani hao toka Kariua. |
Shairi (Ngano) ni moja ya kiungo muhimu katika utengenezaji bia. |
Shairi pamoja na unga wa sembe katika ghala maalum kiwandani hapa. |
Afisa Ubora wa TBL Mwanza, Jeremiah Kimambi akionyesha karatasi maalum ya kuchujia bia ambayo hufungwa kwenye mashine. |
Monodex (Glucose) ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa bia aina ya Castle Light, hapa madiwani wakiionja. |
Asilimia 95 ya bia ni maji hivyo hapa kuna kitengo cha uhifadhi, usafishaji na uchujaji kwa matumizi ya kiwanda. |
Maabara ni muhimu kujua ubora na viwango kusudiwa. |
Madiwani wakishuhudia mitungi maalum ya kuhifadhi bia. |
Chujio dogo. |
Paparazi wa Star Tv Abdalah Tilata naye alijumuika kuzichukuwa taarifa. |
Madiwani wa Kariua wakishuhudia kiwanda jinsi kinavyofanya kazi katika utengenezaji bia na hata uhifadhi kwenye chupa. |
Kuelekea kitengo kingine.... |
Ghala la bia iliyokamilika kwaajili ya kuelekea sokoni. |
Mlima wa mitungi...!! |
Afisa Ubora wa Bia TBL Mwanza Jeremiah Kimambi. |
Wakulima nchini wamehimizwa kulima mazao ya mtama na mahindi kwani soko la nafaka hizo limepanuka kutokana na mahitaji kwa nafaka hizo kutumika katika kutengeneza baadhi ya pombe za Kiwanda cha bia TBL Mkoa wa Mwanza.
Afisa Ubora wa Bia kutoka Kampuni hiyo Jeremia Kamambi amesema kuwa zao la mtama lina nafasi kubwa kuwafanya wakulima kupunguza umasikini kwa kukuza kipato kutokana na kupatikana kwa soko la ndani la uhakika.
Kamambi aliyetwaa tunzo ya Muonjaji bia bora nchini, amesema pamoja na shairi kutumika kutengenezea bia, mazao ya mtama na mahindi yatawafanya wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na Tabora kupanua kilimo chao.(Bofya play)
Baadhi ya Madiwani waliotoa hoja zao. |
Baadhi ya Madiwani wa Wilaya mpya ya Kariua waliotembelea kiwanda hicho wamesema licha ya wakulima wilayani umo kulima zaoidi Tumbaku ipo haja kuwashawishi na kubadili mtazamo wao. (Bofya play)
Halmashauri ya wilaya ya Kariua yenye wakazi zaidi ya laki tatu imeanzishwa kwa Tangazo la Serikali mwaka 2011 na kuzinduliwa agosti 14 mwaka huu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.