Twanga Pepeta,Roma Mkatoliki kupamba Tamasha la
wafanya mazoezi la Vita Malt kesho.
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuhakikisha Watanzania
wanakuwa na afya bora, kinywaji kisicho na kilevi cha Vita Malt, kimeandaa
bonanza maalumu litakalowashirikisha wafanya mazoezi na litakalofanyika katika
mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Vinywaji visivyo na Vileo katika
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Consolata Adam alisema, wameamua kuandaa bonanza
hilo ili kuwakutanisha pamoja wafanya mazoezi wote, ambao mara nyingi
wanafanyia katika vituo maalumu (gym).
Consolata alisema, bonanza hilo
la aina yake kwa Dar es Salaam litafanyika katika Viwanja vya Posta vilivyopo
Kijitonyama kuanzia saa 12 asubuhi hapo kesho (Jumamosi).
“Tumeamua kuandaa bonanza linalowakutanisha
wanamichezo mbalimbali hasa wafanya mazoezi ili kuweza kukutana na kufanya
mazoezi kwa pamoja.
“Siku hiyo katika Viwanja vya
Posta kutakuwa na gym kumi na mbili zilizo maarufu ambazo zitashiriki na
kutakuwa na wakufunzi kumi ambao wataongozwa na mkufunzi wa kimataifa SAAS,”
alisema, huku akidai mtu anatakiwa kwenda tu kwani mazoezi hayo yatakuwa bure.
Alisema, lengo kuu kuu la bonanza
ni kuhamasisha jamii nzima kutambua
umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujenga afya bora za miili yao na pia kujenga
umoja imara wa gym zilizopo nchini.
Consolata alisema, katika
kuhakikisha bonanza hilo linakuwa bora na la kufana jumla ya gym kumi na mbili
zitashiriki ambazo ni Better Life, Genessis ya Kijitonyama, Segerea Gym, Rio
Gym,Genessis ya Kimara, Azula ya Mikocheni na Serena Gym.
Alisema pia baa zilizoshinda
katika kuchoma nyama katika mashindano yaliyofanyika hivi karibuni za Fyatanga
ya Tegeta na Kisuma Bar ya Temeke, zitaonyeshana umwamba kwa kuchoma nyama
bomba kwa kipindi chote hicho.
“Tumeweka burudani za kila aina
kwani kutakuwa na michezo mbalimbali ya kufurahisha kama soka, netiboli, kuvuta
kamba, kukimbiza kuku, Sehemu za watoto kuchezea pia na zawadi nyingi toka Vita
Malt zitakuwepo.”
NaYe Meneja Mawasiliano na
Mahusiano wa TBL, Edith Mushi alisema mbali na hayo kutakuwa na burudani
mbalimbali toka kwa bendi African Stars ‘Twanga Pepeta’ na msanii mkali wa Hip
hop, Roma Mkatoliki sambamba na burudani nyingine nyingi kwa kipindi chote cha
tamasha.
“Hii ni siku ya familia napenda
kuwajulisha watanzania wote na wapenda michezo kote nchini kuwa waje mapema na
familia zao siku ya Jumamosi, hakutakuwa na kiingilio chochote na vinywaji
vyote toka TBL vitakuwepo.
“Lakini pia watu wa kawaida na wa
rika zote siku hiyo hakutakuwa na kikwazo chochote cha kufanya mazoezi, kwani ni
bure kabisa, hivyo nawashauri tufike kwa pamoja ili tuweze kupata pia ushauri
mbalimbali juu ya kupunguza uzito na aina ya mazoezi yanayotakiwa,” alisema.
Vita Malt ni kinyaji
kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.