Akinamama wakiwa tayari kuanza mbio zilizotia fora kuzunguka uwanja mara 10 wakiendesha baiskeli na ndoo za majikichwani. |
Wanaume wakijipinda katika mbio za baiskeli kilometa 210 chini ya Udhamini wa Safari Lager. |
Mshindi wa akinamama waliokimbiza baiskeli kuzunguka uwanja mara 10 Eliza Shilu akipokea zawadi yake toka kwa mgeni rsmi wa mbio za Baiskeli za Safari Lager 2013 zilizofanyika mkoani Shinyanga. |
Ilikuwa ni majira ya saa 1:30 asubuhi mbio za baiskeli za miguu mitatu zilitimua vumbi ndni ya uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga ambapo washiriki walizunguka uwanja mara 30. |
Mbio za baiskeli miguu mitatu zilivyokuwa. |
Hawa ndiyo washindi wa mbio hizo kutoka kulia ni mshindi wa kwanza Ngalu Ngamba, mshindi wa pili ni Peter Thomas na mshindi wa tatu Makende Ndelema. |
Ni mbio za aina yake ambazo zilitia nakshi mashindano ya mbio za Baiskeli na Safari Lager mkoani Shinyanga. |
Kadri muda ulivyokuwa ukisonga umati wa watazamaji ulikuwa ukiongezeka hatimaye ikafikia kipindi uwanja ukafunga kabisa na nyomi ya kutosha. |
Macho yalielekezwa geti kuu. |
Nyomi la wahudhuriaji mbio za baiskeli za Safari Lager 2013 mkoani Shinyanga. |
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 130 wanawake Matha Anthony kutoka wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza akimaliza mbio... |
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kilometa 210 wanaume Masunga Dubha kutoka mkoa wa Mwanza akifurahia kumaliza mbio na ushindi alio upata kwenye mbio hizo. |
Washiriki wengine mbio za baiskeli wanaume. |
Meneja wa TBL Mkoa wa Shinyanga Robert Kazinza akizungumza na maelfu ya watazamaji wa Mashindano ya Mbio za Baiskeli za Safari Lager 2013 zilizofanyika na kufana mkoani Shinyanga. |
We ulikuwa wapi..? |
Au hapa...? |
Wadau wote wa nguvu wa TBL Kanda ya Ziwa wote waliweka maskani mjini Shinyanga. |
Mambo ya Safari lager. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.