ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 9, 2013

FBME WASABABISHA TABASAMU KWA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU WA KITUO CHA AL MASJID IBRAHIM BUTIMBA MWANZA

Meneja wa tawi la FBME Bank Mwanza Ndugu Joseph Gwalugano (kulia) akimkabidhi Imam Abeid Musa Mafuta ya kupikia kwenye hafla fupi iliyofanyika katika msikiti wa Al Masjid Ibrahim Butimba Mwanza.

Jumanne Hassan mfanyakazi wa benki ya FBME Mwanza akimkabidhi mtoto Abdalla, katoni ya amaji ya kunywa

Mfanyakazi wa FBME Bank Mwanza Lena Gahanga (wa pili toka kushoto) akimkabidhi mbuzi mtoto Salima Hamad.

Wafanyakazi wa FBME Bank - Tawi la Mwanza wakiwakabidhi vitu mbalimbali watoto yatima katika msikiti wa Al Masjid Ibrahim - Butimba ikiwa ni maalum kwaajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri

Meneja wa Tawi la benk ya FBME Mwanza akifafanua jambo wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika msikiti wa Al Masjid Ibrahim Butimba huku wafanyakazi wenzake wakimsikiliza

Mfanyakazi wa benki ya FBME Mwanza Mazigo Musiba akimkabidhi Mbuzi mtoto Fatma Fereji kama ishara ya kuwatakia kheri watoto hao na sikukuu ya Eid El Fitri.

Wafanyakazi wa Bank ya FBME tawi la Mwanza wakifurahia jambo baada ya kukabidhi vyakula kwa watoto yatima waliopo msikiti wa Al Masjid Ibrahim Butimba Mwanza

Wafanyakazi wa benki ya FBME tawi la mwanza wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima viongozi wa msikiti Al Masjid Ibrahim - Butima Mwanza.

Wafanyakazi wa Benki ya FBME wakifuatilia tukio, kuanzia kulia ni Lena Gahanga, Rehema Mbalike, Jumanne Hassan, Mazigo Musiba na Peter Nkenguye - Mwan Nzengo

Watoto wa msikiti wa Al Masjid Ibrahim wakitafakari.

Watoto wanaoishi mazingira magumu wa msikiti wa Al Masjid Ibrahim Butimba wakipokea vitu mbalimbali vilivyo tolewa na Benki ya FBME Mwanza kwa ajiri ya sikukuu ya Eid El Fitri ambapo hii imekuwa ni moja ya taratibu za benki hiyo inazozifanya zama za sikukuu mbalimbali.
Blogu hii inatoa pongezi kwa Benki ya FBME kwa utaratibu huu unaofanyika kila mwaka kwa watoto wetu waishio mazingira magumu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.