Dr Madono akimpima Francis Miyeyusho huku Ibrahim Kamwe `Bigright`akishuhudia upimaji huo tayari kwa pambano lake na Mzambia Fidelis Lipupa utakao fanyika leo Dar Live. |
FIDELIS LIPUPA wa Zambia na FRANCIS MIYEYUSHO wa Tanzania |
Ramadhan Kido akipima afya yake katika ofisi za TPBO kwa ajili ya pambano lake dhidi ya Chupaki Chupindi wa Iringa litakalopigwa leo ndani ya Dar live katika kusherehekea sikukuu ua Idd mosi |
Umati wa mashabiki waliojazana katika ofisi za TPBO Tandika wakishudia mabondia wao wakifanyiwa vipimo vya mwisho kwa ajili ya mchezo. |
MABONDIA WAPIMA TAYARI KUZIPIGA HII LEO KUSHEREHEKEA IDD MOSI
Mabondia Francis miyeyusho amewaongoza mabondia waTanzania katika upimaji wa pambano lake dhidi ya bondia Fidelis Lipupa kutoka Zambia katika pambano la kirafiki la kimataifa, linalotarajiwa kupigwa hii leo katika ukumbi wa dar live.
Jana zoezi zima la upimaji liliongozwa na katibu mkuu wa ngumi za kulipwa Ibrahim kamwe akisaidiwa na dr madono .
Mabondia karibu wote waliopima wapo vizuri kwa mapambano yao wakati francis miyeyusho amepata kilogram 55.5 mpinzani wake fidelis lipupa amepata 56 .Ramadhan kido wa dare s salaam amepata kilo 89.7 na mpinzani wake kupata 90.2 .
Pia kutakuwepo na mapambano mengine manne ya utangulizi na mabondia wameuwiana vema na wale kina dada esther na lulu watazichapa kama kawaida
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.