Airtel Rising Stars 2013 yaiva
FAINALI za Taifa za michuano ya vijana chini ya umri wa
miaka 17 za Airtel Rising Stars zimepangwa kuanza kutimua vumbi uwanja wa Kumbu
Kumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Julai 2 kwa mabingwa watetezi Temeke
wavulana kupambana na Kinondoni.
Akizungumza wakati wa
semina elekezi ya Airtel Rising Stars 2013 iliyofanyika Juni mosi katika ukumbi
wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Ofisa Maendeleo wa
shirikisho hilo Bw. Salum Madadi alisema ARS ngazi ya mikoa imepangwa kuanza Juni
15 hadi 29.
Mikoa inayoshiriki
Airtel Rising Stars mwaka huu kwa upande wa wavulana ni mikoa ya kisoka ya
Ilala, Kinondoni na Temeke. Mikoa mingine ni Morogoro Mwanza na Mbeya ambapo
kila mkoa unatakiwa kushirikisha timu sita. Usajili wa timu umepangwa kuanza
rasmi kesho Juni 2 na kumalizika Juni 11.
Kwa upande wa timu za wasichana, alisema, mikoa
itakayoshiriki ni Tanga, Kigoma na Ruvuma na mikoa yote inayoshiriki Airtel
Rising Stars mwaka huu iliwakilishwa kwenye semina elekezi na makatibu wakuu
ambao walipata fursa ya kupitia kanuni na taratibu za michuano hiyo ya vijana.
Upangaji wa ratiba uliofanyika leo ni wa fainali za taifa
pekee kwa kuwa mashindano ya ngazi ya mkoa yataendeshwa na uongozi wa mkoa
husika ikiwa ni pamoja na kupanga ratiba yake.
Kwa upande wa wasichana timu zitakazofungua dimba katika
fainali za taifa ni Ilala na Kinondoni. Kwa ujumla timu 12 zitashiriki fainali
za Taifa, sita za wasichana na sita za wavulana.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa semina hiyo, Meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando alitoa
rai kwa makatibu wakuu wa mikoa kuwa makini wakati wa usajili ili kupata vijana
wenye vipaji ambao wataiwakilisha vema Tanzania kwenye michuanoa ya kimataifa
ya Airtel Rising Stars. Vile vile Tanzania itawakilishwa kwenye klini
itakayofanyika chini ya makocha wa Manchester United.
Alisisitiza alisema nia thabiti ya Airtel Tanzania kuendelea
kusaidia mashindano ya vijana kwa nia ya kuendeleza soka nchini na kuishukuru
TFF na wizara inayohusika na michezo kwa kuyaunga mkono mashindano haya.
Naye mgeni rasmi katika semina hiyo , Katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Msafiri Kondo aliwaomba wadhamini kuendelea
kudhamini michuano hiyo ili vijana wa kike na kiume waweze kufikia malengo yao
katika soka.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.