ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 6, 2013

REDS MISS NYAMAGANA NA WAANDAAJI ANA KWA ANA NA MEYA WA JIJI LA MWANZA KATIKA CHAKULA CHA JIONI.

Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akizungumza na warembo wa kinyang'anyiro cha Reds Miss Nyamagana 2013 katika hafla ya chakula cha jioni ndani ya Gold Crest hotel jijini Mwanza ambapo Meya alitumia nafasi hiyo kuwaasa warembo hao kujizatiti ili kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.

Sehemu ya warembo wanaotaraji kushiriki kinyang'anyiro cha kumsaka mnyange wa Miss Nyamagana 2013 kitakachofanyika tarehe 11/05/2013, wakimsikiliza kwa makini Mhe. Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza kwenye hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Gold crest Mwanza.

Ni wakati wa kujitambulisha kwa warembo.

"Nami naitwaaa...."

"Nami niiii....."

Wote walipata fursa ya kusimama na kujitambulisha hizi ni baadhi tu ya pix...

Mdau namba moja kanda ya ziwa katika masuala ya urembo Mr. John Dotto akitoa shukurani kwa Mstahiki Meya kwa jinsi alivyoshiriki kufanikisha dhima iliyokusudiwa kwaajili ya vijana wa mkoa wake ikiwa ni pamoja na kuhudhuria hafla hiyo yenye lengo la kuboresha uelewa wa washiriki.

Ni warembo walioweza kulinadi vyema eneo la Kanda ya Ziwa. 

Mstahiki Meya akiongoza hatua ya kupata chakula kwenye hafla hiyo nyuma yake ni Meneja wa Club Fusion  Mr. George akifuatiwa na John Dottona wadau wengine nyuma.

Mtangazaji wa Star Tv Abdalah Tilata alipewa shavu kufungua meza ya maakuli kuwakaribisha wanyange wa kinyang'anyiro cha Miss Nyamagana.

Mdau wa habari mkoani Mwanza Peter Fabian kulia 'akimix mapilipili sahanini' 

Mambo ya 'Starter'.

'Vinogesho'

Pichani Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (katikati) akiwa na mwandaaji nambari moja wa mkoa wa Mara Mr. Mkama (kushoto) na Meneja wa Club Fusion Mr. George. 
Miss Nyamagana 2013 inataraji kufanyika tarehe 11/05/2013 katika ukumbi wa hotel ya JB Belmount Mwanza.
na Blogu ya www.gsengo.blogspot.com ni moja kati ya sehemu ya wadhamini wa shindano hilo.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. First off I would like to say superb blog!

    I had a quick question in which I'd like to ask if you do not mind. I was interested to find out how you center yourself and clear your thoughts prior to writing. I have had a tough time clearing my thoughts in getting my thoughts out. I truly do enjoy writing however it just seems like the first 10 to 15 minutes are generally wasted just trying to figure out how to begin. Any recommendations or hints? Appreciate it!

    Here is my blog; garcinia cambogia extract trader joe's

    ReplyDelete
  2. G sengo ni JB Belmonte hotel sio GoldCreast afla ilipofanyika pls badilisha .

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.