Uongozi wa Clouds Media Group kupitia Mkurugenzi wake wa Utafiti na Matukio, Ruge Mutahaba umemtaka msanii wa Bongo Fleva Judith Wambura 'Lady Jay Dee', ajipange na kupokea changamoto badala ya kutafuta mahali kwa kujiegemea kwa kueneza matusi kwao.
Clouds Media leo imefungua mdomo kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miezi mitano tangu Jay Dee alipokuwa akiwarushia makombora kwa madai kuwa wameharibu soko la muziki wa Bongo Fleva sambamba na kuitangaza bendi ya Skylight kwa ajili ya kuiangamiza Machozi Bendi.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam ambapo pia alikuwa akisikika moja kwa moja kupitia redio Clouds, Mutahaba alisema Jay Dee amekuwa akilalamikia mambo mawili ambayo ni bendi ya Skylight na Matangazo yake yaliyoshindwa kurushwa hewani japo alilipia sh 240,000/=
Alisema suala hilo walilimaliza baada ya kumueleza kuwa redio yao haiwezi kukataa matangazo kwa kuwa ndiyo yanayowafanya waendelee kuwa kinara katika suala zima la kuiendesha Clouds Fm.
Zaidi www.gsengo.blogspot.com inakuletea sehemu ya mahojiano live yaliyofanyika leo asubuhi ndani ya Power Breakfast.
SIKILIZA PART ONE:-
SIKILIZA PART TWO:-
SIKILIZA PART THREE:-
Aidha Mr. Ruge Mutahaba ameagiza kuwa siku nzima ya leo ya tarehe 6/05/2013 Redio Clouds FM isipige muziki wa Bongo flavour.
Amesema hii nikuwaeleza wadau wote kuwa Kampuni inajipangia mambo ya kufanya haipangiwi na mtu.
Tupe maoni yako
clouds mmefulia sana acheni majungu kila kukicha.shammeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee on u
ReplyDeleteAnt virus ndo dawa yenu
ReplyDelete