Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Hirani Mansoor akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi. |
Na Peter Fabian
MWANZA.
HALMASHAURI Kuu ya CCM
Mkoa wa Mwanza imefanya uchaguzi na kumchagua Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif
Hirani Mansoor alimaarufu ‘MOIL’ kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha Mkoa huo kwa
mara nyingine tena.
Mbunge Mansoor
amafanikiwa kutetea nafasi hiyo kwa kumshinda Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa (NEC) Wilaya ya Ilemela Israel Mtambalike baada ya kurudiwa uchaguzi huo
jana kufatia kuahirishwa mara ya kwanza wakati ulipofanyika uchaguzi ngazi ya
Mkoa kuwapata viongozi wake kutokana na siku hiyo kuingia giza na wajumbe
kuomba kuahirishwa kumpata mtu katika nafasi hiyo.
Uchaguzi huo
uliofanyika katika ukumbi wa ndani wa uwanja wa CCM Kirumba na kuhudhuliwa na
viongozi waandamizi wa Mkoa ambao ni Mwenyekiti Anthon Dialo na Katibu Joyce
Masunga, Mkuu wa Mkoa Mhandisi Evarist Ndikilo ,Wakuu wa Wilaya Angelina Mabula
(Butiama) na Costantine Kanyansu (Ngara) wajumbe wa NEC wa Wilaya zote na Makada
mbalimbali wakiwemo Wabunge Richard Ndassa (Sumve) na Shanif Mansoor (Kwimba).
Mwenyekiti wa CCM Mkoa
wa Mwanza Dialo awali akifungua kikao hicho alisema kutakuwa na ajenda tano
ikiwemo ya kufungua kikao na ile ya uchaguzi huku zingine zikiwa za kawaida za
kujadili mambo muhimu, kujaza nafasi ambayo awali uchaguzi waOctoba 2012
uliahirishwa na ulipofanyika mwezi Faberuari 2013 wagombea walifungana kwa
kupata kura 32 kila mmoja na hivyo kutopatikana mshindi na kupangwa kurudiwa tena
mei 5 mwaka huu.
“Wajumbe tufanye
uchaguzi wa Katibu wa Uchumi na Fedha ili kukamilisha safu ya uongozi ngazi hii
ya Mkoa na tutumie busara na tuache kufanya kwa shinikizo la mtu kwani wagombea
ni wawili tu watajieleza kwenu na mtawachagua kwa kuwapigia kura za siri ili
kumpata atakayeshinda”alisisitiza Dialo.
Ni mara baada ya kutangazwa matokeo. |
Akitangaza matokeo ya
uchaguzi huo Mwenyekiti Dialo alisema kwamba wajumbe halali waliohudhulia kikao
hicho walikuwa 68 kati ya wajumbe 80 waliotakiwa kuhudhulia hivyo uchaguzi ni
halali kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho,baada ya kupigwa kura Mbunge Mansoor
amejipatia kura 44 na Mjumbe wa NEC Mtambalike amepata kura 24 na hakuna kura
iliyoharibika.
“Safu ya uongozi ngazi
ya Mkoa imekamilika sasa hivyo ndugu wajumbe niwapongeze kwa uamuzi wenu mzuri
wa kumuamini tena Mchumi wetu kuendelea kushika nafasi hiyo na kwa kuzingatia
changamoto zilizopo ndani ya chama na taifa kwa ujumla tumejipanga kutekeleza
majukumu yetu ya uongozi na tunachohitaji kutoka kwenu ni ushirikiano wa dhati
ili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo 2014 serikali za mitaa na 2015
uchaguzi mkuu”alisema Dialo na kushangiliwa na wajumbe wote.
Akizungumza na
waandishi wa Habari baada ya kumalizika kwa kikao hicho Katibu wa Mchumi na
Fedha Mkoa Mbunge Mansoor alisema kwamba
amekuwa ni mtu wa kujitolea kwa kukisaidia chama hicho kwa hali na mali na
wajumbe wameona bado amafaa kuendelea kukitumikia chama kwa miaka mingine
mitano kutokana na kufanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa.
“Wajumbe wamenipa kura
za kutosha hivyo nawapongeza nawaahidi kwenye shughuli zangu za Uchumi
sitowaangusha na ntahakikisha naboresha vyanzo vya mapato na naomba
tushirikiane wanachama wote na viongozi kwa pamoja kukiimalisha chama chetu
huku pia tutajitahidi kupeleka fedha kwenye ngazi za wilaya ili wanachama wetu
ngazi ya Kata, Matawi na Mashina waweze kupata posho za kutekeleza majukumu
yao” alisema
Zaidi msikilize kupitia video hii hapa chini:-
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.