ALIYOSEMA:-
"Tumeanza kuona magazeti yenye affiliation na nchi za jirani yakitumika ku
misrepresent products za TDL"
"Articles ninazozungumzia zilichapishwa tarehe 2 may 2013 na tarehe 6 may 2013,
kupotosha umma, na kupindisha ukweli. kwa sababu mawasiliano ya kisheria
yanafanyika sitataja ni magazeti gani yanahusika, lakini nina uhakika yana
uhusiano mkubwa wa kibiashara na nchi jirani."
"Ushauri wangu ni kuwa magazeti ya Tanzania, yaepukane sana na vitu
vinavyoonyesha kuwa kuna muelekeo wa kurepresent matakwa ya nchi tofauti na
kupuuza matakwa ya kitanzania
Kitendo cha kujaribu kuoanisha brand ya Konyagi na accidents za magari au piki
piki , ni ya upotoshaji mkubwa wa jamii ya kitanzania, kwani hakuna bia, hakuna
pombe za kienyeji au pombe kali. Huu ni uhuni na ujinga mtupu"
"Sisi TDL hatuogopi ushindani, sio ushindani wa humu Tanzania, na nasema
tutaendelea kuuza products zetu zinazozalishwa Tanzania, huko Uganda, Kenya
south Sudan, Rwanda na Burundi, licha ya matatizo makubwa tunayopata
tutaendelea kuwasiliana na mabalozi, wa nchi husika, EAC office na wizara zenye
mamlaka katika kukuza soko la pamoja la Jumuia ya Afrika ya Mashariki, kuhusu
changamoto za kibiashara tunazozipata"
"Kama nilivyozungumza mwanzo sisi hatuzalishi Konyagi tuu, bali tunazalisha
Zanzi cream, Knights, Viceroy brandy , siyo kwa sababu hatuwezi kuagiza, bali
wka kutumia watanzania katika uzalishaji na kuwapa ajira. Msitufananishe sisi
na watu wanaoleta makatoni ya pombe kutoka Ireland au uingereza, sisi tuko
tofauti na mahitaji ya nchi hii tunayajua"
“Raisi wetu Dr Jakaya Kikwete kila siku anasema issue hiyo hiyo, value added ,
value added, mbona masikio yenu mnafunga?”
“Naomba niwaeleze ukienda South Africa leo utaona kila aina ya magari mapya,
utaona Toyota, utaona Nissan utaona Mercedez benz , utaona Kia na kadhalika,
lakini magari yote hayo yanaundwa South Afrika, huwezi kukuta gari
imetengenezewa Singapore, nia ni kuhakikisha kuwa wenyeji wanapata kazi, na
approach yetu TDL ni same”
“Sioni kati ya nyie mtu ambaye anamchukua mtoto wake kumpeleka Nairobi au
Dubai, kumtafutia kazi, wote mnawaleta kwetu, hata leo wengine wananiomba kazi,
kwa hiyo naomba sana mtu akikujaza akili au upumbavu, na wewe jaribu
kuchanganya na akili nzuri za kwako,
Ahsanteni sana”
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.