ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 29, 2013

"NKABAAAA..HILI HAPA PAMBANO LA PASAKA"


COSMAS KIBUGA KUPANDA ULINGONI JUMAPILI

Bondia mwenye makeke mengi na asiyekubali kushindwa ulingoni na huwa tayari kupigana kavukavu Cosmas kibuga anategemea  anategemea kupanda ulingoni jumapili hii ya tarehe 31katika ukumbi wa Texas hall – Manzese, kuzipiga na bondia mkongwe Sweet kalulu katika pambano la kirafiki lakusherehekea  Pasaka. Akilizungumzia pambano hilo Miraji msusa ambae ni muandaaji wa mchezo huo alisema “burudani yetu ni kuangalia ngumi na kushangilia na najua ngumi nzuri zipo katika hawa mabondia wasio na majina na wenye upinzani mkali ,nikaonelea lazima katika sikukuu hii ya pasaka tusiiache ipite hivihivi bila kupata starehe yetu, kusubiri mpaka tarehe 7 april kwenye pambano kubwa la pale ccm mwinjuma-mwanayamala  ni mbali, Nikaafikiana na cosmas kibuga na sweet kalulu ambao ni wapinzani mitaani wamalizie kiu yao hiyo jumapili juu ya ulingo katika pambano la round sita.
Mabondia hao pamoja na wa utangulizi wanategemea kupima  kesho jumamosi saa nne asubui hapohapo katika ukumbi wa Texas hall-manzese

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.