MWANDISHI: NEEMA JOSEPH
Ukweli utabaki
palepale kwamba afya bora ni muhimu kwa binadamu kuliko kitu kingine chochote hapa duniani. Siku zote
binadamu anapo ishi duniani kila kukicha anategemea awe mzima ndipo atakapoendelea na shuguli zake kwa sababu mtu hawezi kupanga
mipango ya kesho kama mwilini kwake kuna maradhi.
Ilikuwa
ni jioni ambapo nilipiga kambi
katika nyumba ya Cosmas Bonifance, mzee ambaye
anaishi na wake wawili na kwa
wakati huo alikuwa kwa bi
mkubwa akiwa ameenda
kiumtembelea na kumpelekea matumzi .
hapo ndipo
mzee huyo alipoanza mazungumzo
name kwa kuniambia ushiriki wake kikamilifu
katika huduma ya
ushiriki wa uzazi wa afya
kwa familia yake
yenye wake wawili, kwa
ujumla mzee Cosmas amekiri kushiriki
kikamilifu kwenye huduma ya
uzazi wa afya baada ya
kupata elimu na kuhudhuria
semina mbalimbali tofauti na hapo
awali.
Kwa
sasa anakwenda kliniki
na mkeo na kushiriki hatua
zote za tangu
mwenza wake anapoanza kuhudhuria
kliniki hadi anapojifungua ikiwa na pamoja na kupima vipimo
vinavyohitajika wakati mama akiwa
mjamzito.
“Kabla ya
kupewa elimu ya ushiriki
wa huduma ya uzazi ya
afya mke wangu
hakuthubutu kuniambia juu
ya ushiriki wangu
wakati wa ujauzito wake na
hata mila na desturi za kabila letu
la wasukuma hazikuruhusu mwanaume
kushirikishwa kwenye afya
ya uzazi” alisema bwana
Cosmas.
Kwa
hivi sasa bwana Cosmas
anaishi na wake zake wawili na
amekuwa akishiriki vyema katika huduma
ya afya
ya uzazi kwa wote licha ya mke wake mkubwa
aliyemtaja kwa jina la luncy
Magesa kutokuwa na mtoto kutokana
na kila anaposhika mimba, mimba
uharibika lakini yeye amekuwa mshiriki
wa karibu katika kufahamu
chanzo cha tatizo hilo.
Sheria ya masuala ya
uzazi na ushiriki wa mwanaume inasisitiza
mwanaume kushiriki katika huduma
ya afya ya
uzazi kikamlifu lakini wanaume wengi
hawaijui sheria hiyo
hali inayosababisha ugumu wa kuwaomba waajiri wao ruksa
ya kumsindikiza mke/wake kliniki
na baadhi yao wanaoijua
wansingizia kuwa wananyimwa ruksa
na waajiri wao kuwasindikiza wake zao.
Lengo la tano
la millennia linasisitiza kupunguza
vifo vya kinamama wajawazito kwa
robo tatu ya
vifo kati ya mwaka 1990 hadi 2015 sanjali
na lengo la
sita la kukinga maambukizi
ya virusi vya ukimwi, malaria na magonjwa
mengineyo.
Sera ya afya
ya Tanzania ya mwaka 2003
iliyosainiwa na waziri wa afya
wakati hulo Anna Magreth
Abdallah moja ya
lengo lake kati ya
malengo tisa ni kupunguza
maradhi kwa wakina mama wajawazito na watoto
na kuongeza umri wa kuishi.
Takwimu za shirika la
chakula duniani (FAO) zinaonyesha kuwa
wanawake huzalisha asilimia 60 na 80 ya chakula chote katika nchi
zinazoendelea.wanawake wanatoa mchango
mkubwa kama wazalishaji wakuu wa chakula
katika ngazi za familia hatua ambayo imeanza kutambuliwa na kudhaminiwa na
vikao mbalimbali kitaifa na kimataifa.
Serikali kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali(NGOS) imefanya
kazi ya kuondoa vipengele vinavyo bagua
sheria zinazotumika ambazo hazitoi haki
na uhuru wa wanawake ,Aidha, serikali imepitisha sheria kadha katika
kutoa upendeleo kwa mwanamke
mfano”sexual offences special provision Act of 1998, land law Act of 1999, na
village land Act1999.
Sheria ya kwanza itawalinda
wanawake, wasichana na watoto kutokana na kunyanyaswa kijinsia na
kutendewa matendo mabaya .katika
maeneo mbali mbali, mathalani mkoa wa Arusha, familia nyingi uimara wake
umewezeshwa na wanawake, ambao ndio walezi
na wenye kutafuta kipato kwaajili ya kutunza familia.
Ushiriki wa wanaume katika swala zima la afya ya uzazi mkoa wa mwanza umeongezeka kwa asilimia 24 kwa mwaka 2011 haya yamebainishwa na katibu mkuu
wa mkoa
hospitali ya seketure mwanza Bw, Danni
temba.
Mara
nyingi wanawake wamekuwa wahanga wa tabia , mila,
na desturi zenye
athari katika afya
ya uzazi kama ukeketaji kwa
wanawake, kudhalilishwa kingono
, unyanyasaji wa kijinsia,
ukahaba, kulazimishwa kuolewa
a u kuoa mapema
na utumiaji wa
madawa ya kulevya.
Wanaume waache kuwanyanyapaa
wenza wao, ubepari, mila, na desturi walizo nazo waziiache, afya ya mama
mjamzito ni muhimu kuliko kitu kingine chochote
duniani, hinyo wanaume wadhubutu kwani nia, uwezo na nguvu wanazo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.