ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 25, 2013

AMOUR MZUNGU AMTISHIA NYAU MARWA

Bondia mwenye makazi yake kisiwani unguja Amour Said 'mzungu'  (kushoto) akiwa na marehemu Kizakinene (kulia).


 'Mzungu' amejitapa kumpiga vibaya na kumstaafisha ngumi bondia mkongwe aliyewahi kuchukua medali nyingi tofautitofauti katika ngumi za ridhaa na kuwa bingwa katika ngumi zakulipwa Joseph Marwa katika  pambano litakalofanyika katika ukumbi wa  CCM Mwinjuma-Mwananyamala april  7, Mzungu aliendelea kwa kusema kuwa marwa umri umekwenda na anakili kama Marwa amemkaribisha katika ngumi na sasa wanapiga na aliyekuwa mwalimu wake na sasa ni zamu yake  kumfundisha kwa kumchapa bila huruma anataka akimaliza kazi na Marwa amtafute kule aliko bondia Mchumiatumbo ili amwonyeshe kwamba yeye ni bora katika ngumi za uzito mkubwa wa juu hapa nchini.  

Pambano la Amour Mzungu na Joseph Marwa litapigwa kwa raundi nane kuwasindikiza wadogo zao wanaochipukia  kwa kasi Issa Omar na Shaban Madilu. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.