ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 25, 2013

MICHEZO MASHULENI ITASAIDIA KUONGEZA MAHUDHURIO

Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Mwanza Mwalimu Hamisi Maulid akizungumza na wadau wa michezo mkoani humo katika semina ya mafunzo michezo mbalimbali iliyofanyika ukumbi wa ofisi za mkoa.

Semina ya mafunzo ya utoaji taaluma ya michezo kwa waalimu, makocha na wadau wa michezo toka shule mbalimbali yamefanyika jijini Mwanza.

Mafunzo hayo yamekuja yakiwa na lengo la kuwakomaza waalimu ambao ni wasimamizi wakuu wa taaluma za michezo mkoani Mwanza ili kuzalisha vipaji vyenye misingi imara tangu awali.

Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Mwanza Mwalimu Hamisi Maulid anazungumza na Sports Xtra na hapa anafafanua zaidi kwa kina juu ya semina hiyo.

Sikiliza kwa kubofya Play..

Jumla ya washiriki 36 wakiwemo maafisa michezo wa Halmashauri, wakuu wa vyuo vya michezo Butimba na Chuo cha maendeleo ya Michezo Malya, viongozi wa vyama vya michezo ya riadha, mpira wa miguu (wanaume na wanawake) pamoja na waandishi wa habari wamehudhuria semina hiyo.

Washiriki kwa umakini zaidi seminani.

Jumla ya washiriki 36 wakiwemo maafisa michezo wa Halmashauri, wakuu wa vyuo vya michezo Butimba na Chuo cha maendeleo ya Michezo Malya, viongozi wa vyama vya michezo ya riadha, mpira wa miguu (wanaume na wanawake) pamoja na waandishi wa habari wamehudhuria semina hiyo.

Neno la shukurani kutoka kwa Afisa Michezo wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza kuwakilisha wanasemina walioshiriki.

Washiriki wakiwemo maafisa michezo wa Halmashauri, wakuu wa vyuo vya michezo Butimba na Chuo cha maendeleo ya Michezo Malya, viongozi wa vyama vya michezo ya riadha, mpira wa miguu (wanaume na wanawake) pamoja na waandishi wa habari katika picha ya pamoja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.