ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 25, 2013

MKUTANO WA WADAU WA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI TANZANIA WAFANYIKA MWANZA


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akifungua Warsha ya siku mbili ya wadau viongozi wa maeneo yenye Hifadhi za Taifa nchini unaofanyika Hotel Gold Crest jijini Mwanza ukihuduriwa na Wakuu wa mikoa na wilaya zilizo na hifadhi, Wakurugenzi na viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza katika maeneo mbalimbali yenye hifadhi hapa nchini.  


Pichani meza ya mbele ni wakuu viongozi kutoka wilaya ya Magu waliohudhuria warsha hiyo.


Tanzania ina jumla ya hifadhi 15 na siku si nyingi inategemea kuongeza hifadhi moja zaidi pindi itakapo kamilika hifadhi ya kisiwa cha Saa nane iliyo ndani ya ziwa Victoria jijini Mwanza.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA amesema kuwa kwa kutambua kuwa ushirikiano wa viongozi na wananchi waliokuwa wakimiliki maeneo hayo kabla ya kuwa hifadhi au wananchi waishio pembezoni mwa hifadhi hizo bila ya kushirikiana nao lengo la hifadhi halitofanikiwa.

Hivyo Warsha hiyo imeanzisha sera ya ujirani mwema ambapo TANAPA itaendelea kudumisha ushirika wa moja kwa moja na wananchi hao katika masuala mbalimbali ya ulinzi na utunzaji mazingira. 


Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye warsha hiyo, hawa ndiyo wenye dhamana ya kusimamia wananchi wanaozunguka hifadhi mbalimbali nchini pamoja na shughuli za utalii ndani ya hifadhi.


Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Kondisaga akiwakaribisha wadau washiriki wa Warsha hiyo hasa ikizingatiwa kuwa kusanyiko hilo la warsha linafanyika ndani ya Gold Crest iliyo wilayani kwake.


Meza ya wadau toka wilaya ya Ilemela wakiongozwa na Mbunge Highness Kiwia (kulia), Mkurugenzi wa wilaya (katikati) na Mkuu wa wilaya hiyo Amina Masenza.


Lengo la warsha ni kufanya tathimini kwa ujumla juu ya ushirikiano baina ya viongozi na wananchi wa maeneo ya hifadhi  ambapo maoni mbalimbali yanategemewa kuwasilishwa ili kuimarisha ushirikiano kwa manufaa ya wananchi ambao TANAPA inalenga kushirikiana nao katika shughuli za uhifadhi hivyo kufaidika.


Hata hivyo sekta ya uhifadhi nchini inakabiliwa na changamoto nyingi za uharibifu wa mazingira kama vile vyanzo vya maji kuharibiwa, mapito ya wanyama, changamoto za migongano ya wanyama pori na shughuli za maendeleo ya binadamu.


Wadau kutoka wilaya ya Serengeti. 


Changamoto nyingine zilizo tajwa ni pamoja na Ujangili na migogoro ya ardhi.


Sehemu tu ya wanahabari kwenye semina hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.