Afisa Mauzo wa Airtel bi Theresia Kimaro Akiongea na wateja juu ya huduma ya Airtel yatosha wakati Airtel walioko Magomeni na kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali ikiwemo ya Airtle yatosha |
AIRTEL YATOSHA YAENDA MIKOANI
*Uzinduzi wa huduma Yatosha wafanyika rasmi Mwanza ,
Kanda ya ziwa waanza kupiga
simu kwa gharama nafuu Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kusambaza huduma ya Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali nchini baada ya kuzindua huduma mpya ya punguzo la upigaji simu maarufu kama Airtel YATOSHA katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Airtel sasa imeanza kuitambulisha huduma hiyo kwa wadau na wateja wake katika mikoa mbalimbali nchini ili waweze kunufaika nayo Huduma ya Airtel Yatosha inamuwezesha mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.
Akionge wakati wa utambulisho wa huduma ya Airtel Yatosha kwa wadau wa Airtel jijini Mwanza, Meneja wa kampuni hiyo kanda ya ziwa Ally Maswanya alisema" Tumeamua kushusha gharama hizo kutokana na maagizo ya mamlaka ya mawasiliano ambayo iliagiza gharama za simu kushushwa kutoka shilingi 112 kwa dakika hadi shilingi 34.92. kwa sasa huduma ya airtel yatosha ina punguzo la hadi asilimia 88 na inalenga kurahisisha mawasiliano kwa wateja wa hali zote kwa kuwawezesha kutumia kiwango kidogo cha fedha kupata muda wa maongezi wa kuanzia dakika 10 kupiga mitandao yote ,meseji bila kikomo na huduma ya internet".
Punguzo hilo la bei linatoa faraja kwa watumiaji wa mtandao huo kwa kuwa litawawezesha kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho walikuwa wakikitumia hapo awali. Aliongeza Maswanya.
Akiongea wakati wa halfa ya uzinduzi Mteja wa Airtel na mkazi wa Mwanza Bi Agness Emmanuel alisema" Aritel yatosha sasa ndio suluhisho la mawasiliano ya simu ya bei nafuu, tunashukuru Airtel kwa kutoa vifurushi vingi na vya bei nafuu vinavyokidhi adha ya sisi wateja huduma hii itatuletea urahisi wa mawasiliano bila haja ya kuwa na simu nyingi na usumbufu wa kuwa na line nyingi. Kwakweli Airtel yatosha itakuwa ni mkombozi katika mawasiliano.
Kwa upande wake Bwana Brighton Maisel moja ya wateja waliohudhuria uzinduzi huo alisema"ni kwa muda mrefu sasa mawasiliano ya simu za mkononi kwenda mitandao mingine yamekuwa ya gharama za juu hivyo nashukuru sana serikali kuweka sheria ya kupunguza bei kati ya mitandaa na Airtel kwa kutii na kuja na Airtel yatosha ambayo sasa inatuwezesha kuwasiliano kwa bei nafuu na wateja wote wa mitandao ya simu za mkononi mingine"
Airtel wiki hii pia bado itaendelea kufanya uzinduzi wa huduma hii katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Arusha, Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa kuwafikia watanzania na kuwaelimisha kuhusu huduma hii ya Airtel Yatosha
Kujiunga na huduma hii mteja anatakia kupiga *149*99# na kuunganisha moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchagua kifurushi anachokipenda na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.