ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 24, 2013

MAPOKEZI YA NABII ELIYA ADANI 2 JIJINI MWANZA YALIVYOKUWA JANA

Msafara wa magari kwa mapokezi ya Nabii Eliya ADANI ndani ya jiji la Mwanza kuelekea katika kanisa la The Pool Of Siloam lililoko katika ukumbi wa Vijana Social Kirumba tukio lililojiri jana.

Msafara wa magari kwa mapokezi ya Nabii Eliya ADANI ndani ya jiji la Mwanza kuelekea katika kanisa la The Pool Of Siloam lililoko katika ukumbi wa Vijana Social Kirumba, ujio wa Nabii umekuja kwaajili ya kumpaka mafuta na kumsimika rasmi mchungaji wa kanisa hilo jijini hapa. 

Huyu ndiye Nabii Eliya ADANI na hapa akiingia katika kanisa la The Pool Of Siloam huku mapokezi yakiendelea.

Nabii Eliya ADANI wa kanisa la The Pool Of Siloam na mapokezi mazito.

Hivi ndivyo waumini wa kanisa hilo walivyokuwa wamejiandaa na njia ya kuelekea madhabahuni.

 Waumini wa Kanisa la The Pool Of Siloam wakiwa katika shamrashamra za kumpokea Nabii Eliya ADANI kanisa hilo kwenye Ukumbi wa Vijana Social Kirumba Mwanza ujio wa Nabii umekuja kwaajili ya kumpaka mafuta na kumsimika rasmi mchungaji wa kanisa hilo jijini hapa.

Nabii Eliya ADANI akitoa neno kwa waumini wa kanisa la The Pool Of Siloam waliofurika jana kumpokea, ujio wa Nabii umekuja kwaajili ya kumpaka mafuta na kumsimika rasmi mchungaji wa kanisa hilo jijini hapa, shughuli ambayo itafanyika Jumapili (leo).

Waumini wa kanisa la The Pool Of Siloam jijini Mwanza na shamrashamra zao wakiimba kwa furaha....

Meza kuu na nabii kwenye ibada hiyo iliyofanyika jana.

Kwaya ikiabudu jukaani.

Nao walioguswa hawakusita kusimama kuimba kwa kumsifu Mungu. 

Vuvuzela jadi ya shangwe za mwafrika....!!!!

Kwaya jukaani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.