ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 24, 2013

UONGOZI WA TAASISI YA ALJAZIRA ISLAMIC CENTRE UKEREWE WAKANUSHA HABARI ZA KUJIHUSISHA NA UGAIDI, WATOA SIKU 7 KWA GAZETI LA MTANZANIA KUKANUSHA KWA MAANDISHI MAKUBWA TAARIFA ILIZOTOA LA SIVYO ITACHUKUA HATUA ZA KISHERIA.


Shekh Jabir Katula ambaye ni mmoja kati ya waasisi wa kituo cha Aljazira Islamic akizungumza na waandishi wa habari huku akishuhudiwa na baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali.
Uongozi wa Taasisis ya Al Jazira Aslamic Centre umekanusha habari ilizotaja kuwa ni za uongo, uzushi na ufitini zilizochapishwa na gazeti la Mtanzania toleo la tarehe 13 februari 2013 na toleo la tarehe 20 februari 2013 zikikitaja kituo hicho kufadhiliwa na makundi ya Al-Qaeda na Al-Shabab yanayoaminika kuwa na mtandao mkubwa wa ugaidi duniani.

Mkurugenzi  wa Chuo Cha Aljazira Islamic Centre kilichopo Ukerewe, Shekhe Ramadhani Mazige akitoa tamko rasmi la kukanusha habari za chuo chake kuhusishwa na taarifa za kufundisha ugaidi na kuwa na mahusiano na vikundi haramu. 

Zaidi sikiliza Tamko..
Aidha kituo hicho kimesikitishwa na taarifa hizo na kutia mkazo kulitaka gazeti hilo (Mtanzania) kuomba radhi kabla ya siku saba kutokana na demand note waliyoitoa, kinyume na hapo taasisi hiyo imesema kuwa itachukuwa hatua zaidi za kisheria.
Kusanyiko lililofika kushuhudia tamko.

Shekhe Mohamed Salum Mbala Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mwanza.
"Habari iliyotangazwa imetustusha sana imetudhalilisha, imetuudhi ni taarifa ambayo haikufanyiwa utafiti, imevunja heshima ya waislamu sio wa Mwanza Tanzania pekee bali dunia nzima, tunasema wazi kuwa sisis waislamu tunapenda amani na tuko kwaajili ya kuitangaza amani na hatuko tayari kuvurugwa kuipoteza amani ya nchi hii"

"Kwa kweli tunalaani sana udhalilishaji huu tunaomba mwandishi wa habari hizo atoe ushahidi na hatutokubali kama hatotoa ushahidi" 
Shekhe Musa Kunenge ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Chuo cha Aljazira Islamic Centre Ukerewe amesema kuwa chuo chake kilipata idhini ya waislamu kwenye msikiti, kisha kikafuata njia zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kupata kiwanja hatimaye usajili na shughuli zote zinatendeka kwa haki na uhalali na wala kituo hicho hakijihusishi na yale yanayotajwa kwenye magazeti kukichafua chuo hicho. 

Kwa upande wake Shekhe wa Msikiti wa Ibadhi mkoani Mwanza, amesema kuwa mara baada ya taarifa hizo kuzagaa kufuatia kuandikwa na vyombo vya habari hususani gazeti la Mtanzania kumezuka athari nyingi sana kwa jamii ya waislamu hata baadhi ya wananchi kulalamika kukosa huduma zilizo sehemu ya haki za binadamu hivyo ameitaka Serikali kutofumbia macho viashiria vyote na kutotoa nafasi kwa yeyote anaye nuia kuvuruga amani ya nchi hii. 
Sehemu ya kusanyiko lililofika kushuhudia tamko.

Sehemu ya kusanyiko lililofika kushuhudia tamko.

Pichani ni Wahitimu wa Chuo cha Aljazira Islamic Centre kilichopo wilayani Ukerewe kiasi cha kilomita mbili toka Nansio mjini, ambapo uongozi wa Chuo hicho umekanusha kabisa taarifa za hivi karibuni zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania kwa Chuo hicho kuhusishwa na utoaji mafunzo ya kigaidi ikiwa ni pamoja na kufadhiliwa na makundi ya kigaidi. 

Pichani ni Viongozi, walezi pamoja na walimu wa Chuo cha Aljazira Islamic Centre kilichopo wilayani Ukerewe katika picha ya pamoja kwenye moja kati ya maafali , ambapo uongozi wa Chuo hicho umekanusha kabisa taarifa za hivi karibuni zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania kwa Chuo hicho kuhusishwa na utoaji mafunzo ya kigaidi ikiwa ni pamoja na kufadhiliwa na makundi ya kigaidi. 

Pichani ni Wahitimu wa Chuo cha Aljazira Islamic Centre kilichopo wilayani Ukerewe wakiwa na zawadi zao kwenye moja ya maafali chuoni hapo. Uongozi wa Chuo hicho umekanusha taarifa za hivi karibuni zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania kwa Chuo hicho kuhusishwa na utoaji mafunzo ya kigaidi ikiwa ni pamoja na kufadhiliwa na makundi ya kigaidi. 

Moja ya majengo ya Chuo cha Aljazira Islamic Centre kilichopo wilayani Ukerewe kiasi cha kilomita mbili toka Nansio mjini.

Mbele ya moja ya majengo ya Chuo cha Aljazira Islamic Centre kilichopo wilayani Ukerewe kiasi cha kilomita mbili toka Nansio mjini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.