ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 7, 2013

AIRTEL YAZINDUA PROMOSHENI YA PATA MUDA WA MAONGEZI MARA MBILI KUPITIA AIRTEL MONEY


cid:image002.jpg@01CE0514.E1FF41D0
Airtel yazindua promosheni ya pata Muda wa maongezi mara mbili kupitia Airtel money
·         Wateja kupata salio mara mbili kila anapotuma pesa kupitia Airtel Money
·         Ni kwa wateja wa malipo ya awali nchi nzima
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua promosheni mpaya ya Airtel Money ambapo wateja wakel watapata muda wa maongezi mara mbili ya gharama watakazotozwa kwa kutuma  pesa na kupata wateja muda wa maongezi kulingana na ada ya makato pale wanapotoa pesa  kwa kupita huduma ya  Airtel money.

Akizungumza kuhusu promosheni hiyo, Meneja Uhusiano Jackson Mmbando alisema” Tumewawezesha wateja wetu kutumia huduma ya Airtel money na kufanya miamala mbalimbali ya pesa huku tukisogeza huduma za kifedha karibu na makazi na sehemu zao za  kazi , leo tunayofuraha kuwazawadia wateja  wetu waliojisajili nchini nzima muda wa maongezi mara mbili ya gharama watakazotozwa kutuma pesa kupitia Airtel money na pia tunawapa muda wa maongezi kulingana na ada watakayotozwa kutoa pesa pale watakapo toa pesa kupitia Airtel money. Bonus hii ya muda wa maongezi itatumika  kupiga simu Airtel kwenda Airtel siku nzima , kwa siku nzima hadi saa sita usiku.”

“Tunaendelea kuboresha huduma yetu ya Airtel money na kuendelea kutoa suluhisho la huduma za kifedha hasa katika maeneo yenye changamoto ya huduma za kibenki. kwa kupitia mtandao wetu mpana ulioenea zaidi tuna wawezesha watanzania nchni nzima hasa wa maeneo ya vijijini kupata huduma za fedha zilizo salama , nafuu na gharama nafuu kupitia Airtel Money.

Promosheni hii ya pata muda wa maongezi itaondoa Kampeni ya  bure,  na kuanzia sasa wateja wa Airtel watazawadia muda wa maongezi kila wanapotuma na kupokea pesa kupitia huduma ya Airtel Money”. Aliongeza Mmbando.

Airtel bado inaendelea kutoa huduma za mawasiliano za simu zenye ubora na gharama nafuu , kwa sasa wateja wa Airtel wa malipo ya Awali wanatuma ujumbe mfupi was ms kwa shilingi moja mara baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kwanza kwa shilingi 125na kupiga simu kwa senti 10 mara baada ya dakika mbili za mwanzo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.