Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Shule ya Sekondari Loyola ya jijini Dar es Salaam jana. |
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Loyola ya jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali ndani ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Shule ya Sekondari Loyola. |
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Loyola ya jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali ndani ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Shule ya Sekondari Loyola. |
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Loyola wakionesha ubunifu wa mavazi katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Shuleni hapo. |
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi akizungumza na wanahabari kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Shule ya Sekondari Loyola. |
Na Mwandishi wa
Thehabari.com
KAIMU Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Lilian Liundi amesema
wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri na mfano wa kuigwa katika maeneo
mbalimbali endapo watajengewa mazingira na kuandaliwa mapema tangu wawapo
shuleni.
Bi. Liundi ambaye pia ni
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya TGNP ametoa changamoto hiyo leo
katika Shule ya Sekondari ya Loyola ya jijini Dar es Salaam alipokuwa mgeni
rasmi katika maadhimisho ya siku ya mwanamke shuleni hapo.
Akizungumza na umati wa
wanafunzi wasichana wa shule hiyo na wageni anuai waalikwa, alisema tafiti
nyingi zilizofanywa zinaonesha kuwa wasichana wanapoandaliwa mazingira mazuri
ya elimu wanafanya vizuri ukilinganisha na wavulana.
Aidha aliongeza kuwa kwa
sasa zipo shule zinazochukua wasichana pekee ambazo zimekuwa zikifanya vizuri
zaidi jambo ambalo linaonesha wazi mazingira mazuri yakijengwa jamii hii
inaweza kuinuka na kuwa mfano mzuri.
Alisema kwa sasa
vishawishi na changamoto anuai zilizopo katika shule nyingi ndio kikwazo kwa wanafunzi
wa kike kufanya vizuri, hali ambayo ikifanyiwa kazi kiufasaha mabadiliko
kimafanikio kwa kundi hilo yanaweza kutokea.
Hata hivyo alisema
tafsiri iliyojengeka ya kwamba wanafunzi wa kike wanaogopa masomo ya sayansi si
sahihi kiuhalisia, kwani mazingira ambayo wanafunzi hawa wanakumbana nayo ndio
kikwanzo katika mafanikio yao kimasomo.
“Mfano shule nyingi za
kata ni za kutwa wanafunzi hasa wasichana wanakaa mbali na shule, wanalazimika
kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni…wanakumbana na changamoto nyingi
njiani hivyo wanajikuta wanashindwa kufanya vizuri au kukatishwa kabisa masomo
yao,” alisema Bi. Liundi.
Aliongeza kuwa eneo kama
hili, vyombo husika vikiangalia sheria na sera zinazojenga mazingira mazuri kwa
makundi yote, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika
vizuri wasichana wanaweza kuingia katika ushindani kwa fursa zilizopo.
Kwa upande wake
mwanafunzi Grace Ntambi wa kidato cha tano wa shule hiyo aliiomba serikali
kuendelea kutoa elimu kwa mikoa ambayo bado inaendeleza mila potofu za kumbagua
mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kuelemea kwenye mfumo dume, ili kuangamiza
vitendo hivyo.
“Na hii ianzie pia
katika ngazi za familia kuna kila sababu ya kuondokana na mila potofu za kwamba
mtoto wa kike hana haki ya kupata elimu kama ilivyo kwa mtoto wa kiume…tuwatie
moyo wasichana kwani wanaweza,” alisema mwanafunzi huyo.
Katika hafla hiyo pia
TGNP ilipata fursa ya kutoa mada mbalimbali za masuala ya wanafunzi kujitambua
kwa hatua anuai ikiwa ni pamoja na kutoa ushuhuda ya kwamba wanawake wanaweza
wakiamua kufanya hivyo kwa kila hatua wanayopiga.
Imeandaliwa na Mtandao
wa Thehabari.com (www.thehabari.com)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.