ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 2, 2013

MAZISHI YA SAJUKI SASA KUFANYIKA IJUMAA NA SIYO KESHO: CHENI ASEMA SAJUKI ALIKUWA MWANAUME MWENYE MOYO WA AINA YAKE.


Kwa taarifa zilizopatikana hivi punde kupitia kituo cha Redio Clouds Fm zinasema kuwa mazishi ya msanii aliyekuwa akiugua kwa muda mrefu, mwigizaji mahiri Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia leo majira ya saa moja asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili yatafanyika Ijumaa na si kesho (alhamisi) kama ilivyotangazwa awali. 

Simon Simalenga ambaye yuko eneo la msiba huo hapa anazungumza na E.Kibonde wa Jahazi.. Msikilize kwa kubofya Play..



Kifo cha Sajuki kwa wasanii kimefungua dimba kwa mwaka 2013, huku ukiwa na kumbukumbu za kuondokewa na wasanii watano katika kipindi cha mwaka 2012, akiwamo Steven Kanumba, Sharomillionea na wengineo.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. 
Amen

Tupe maoni yako

1 comments:

Note: Only a member of this blog may post a comment.