Mtoto Samwel Mlope. |
Unaweza kujiuliza ni nini ambacho kimetokeza katika mgongo wa mtoto huyu?.Mtoto Samwel Mlope mwenye umri wa miaka kumi na moja(11) ambaye ni mkazi wa Mahenge ndani ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.Mtoto huyu alianza kuumwa mwaka 2001 ambapo alianza kusumbuliwa na tatizo la moyo kuwa na tundu.
Kwa mala ya kwanza kabisa alipoanza kusumbuliwa na tatizo hili mama yake ambaye ni Bibi Amina Ally alimpeleka katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma na kuambiwa ampeleke mtoto katika hospital ya Taifa Muhimbili na baada ya kufika muhumbili ndipo alipoambiwa kuwa mtoto Samwel anasumbuliwa na tatizo la kuwa na tundu kwenye moyowake.
Afya ya mtoto Samwel siyo nzuri kabisa na ndio maana anashidwa hata kupata masomo na kushindwa kutimiza malengo ambayo aliyakusudia.
Na huyu ndiye mama mzazi wa mtoto Samwel Mrope Bibi Amina Ally ambaye anajishughulisha na kazi za ndani ili aweze kujipatia pesa kwa ajili ya kujikimu kimaisha yeye pamoja na mwanae Samwel. |
Alisema kuwa "baba wa mtoto Samwel aliondika muda mrefu sana uliopita kuelekea machimbo kwa ajili ya kutafuta na mpaka hii leo hajarudi na hawafahamu yupowapi.
Bibi Amina alisema kuwa "ninawaomba watanzania na ambao sio watanzania wote kwa ujumla waweze kunisaidia ili mwanangu Samwel aweze kwenda nchini India na kupata matibabu kwani mwanangu anapata shida sana"na hatimaye aliweza kuzitowa namba zake za simu kwa watu ambao watajitokeza kutoa msaada kwa mtoto Samwel ambazo ni 0752732290.
Kwa hisani ya Blog ya Demasho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.