Na Shomari Binda
Musoma,
HOSPITALI ya mkoa wa Mara iko katika hatari kubwa ya kukubwa na
milipuko ya magonjwa mbalimbali yakiwezo ya kuhara kutokana na wodi zake nyingi
kukosa vyoo jambo ambalo linasababisha wagonjwa kujistili ovyo
ndani na nje ya wodi hizo.
Mwandishi wa habari hizi juzi alishuhudia kinyesi kingi kikiwa
kimetapakaa nje ya wodi hizo huku wagonjwa wakitumia vyombo kama madishi na
majagi kwaajili ya kuhifadhia mkojo.
Baadhi ya watu ambao wanaguza ndugu zao katika wodi namba saba na
tatu katika hospitali hiyo,waliliambia gazeti hili kuwa wagonjwa wanalazimika
kujisitili nje ya wodi hizo na kusababisha kutapakaa ovyo kwa
kinyesi hicho.
Walisema hivi sasa wanalazimika kununua vyombo kama madishi na
majagi kwaajili ya kuhifadhi mkojo wa waguzi wa wagonjwa na wagonjwa
hasa nyakati jambo ambalo walisema linaweza kusababisha milipuko mikubwa ya
magonjwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kukabili hali hiyo.
“Wewe ona uwanja wote huu umejaa kinyesi hayo madishi uliyaona
humu ndani si kwamba yamehifadhi maji bali ni mkojo kwani wodi hii na zingine
zote hazina vyoo”alisema mama mmoja juzi usiku wakati akizungumza na MTANZANIA.
“Sehemu hii ambayo unaona kuna marundo marundo ya mchanga hicho ni
kinyesi kimefukiwa na watu asbihi wanakaa katika maeneo haya hivi unategemea
nini kama si magonjwa…kweli sehemu ya afya kama hii hali inakuwa hivi je hapa
tunajifunza nini sisi”alihoji mzee Ramadhan Said.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo ya mkoa wa Mara Dk Iragi
Ngerageza akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alikiri wodi hizo kukosa
vyoo kwa madai kuwa majengo hayo ni ya muda mrefu na kwamba tayari mhandisi wa
ujenzi wa mkoa ameombwa kuandaa michoro mipya ya kuwezesha ujenzi wa mfumo
mzima wa maji machafu na vyoo hivyo.
“Ni kweli kabisa hayo unayouliza ndio yapo katika hospitali
hii,kama unavyojua mimi ni mgeni nimekuja juzi nilipokuta hali hii nilitishika
sana sana hivyo ilinibidi kumwite mhandisi wa mkoa kwaajili ya kuona hatua za
haraka za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuandaa michoro ya kuwezesha kujenga
mfumo mzima wa maji machafu na vyoo hivyo kwani majengo haya ni ya muda
mrefu”alisema mganga huyo mfawidhi.
Hata hivyo alisema baada ya waziri wa Afya na Usatawi wa jamii
kuteua wajumbe wa bodi ya uendeshaji wa hospitali hiyo ambayo inatarajiwa
kuzinduliwa kesho,itasadia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto nyingi
zinazoikabili hospitali hiyo hivi sasa.
Tupe maoni yako
Maybe you should produce alterations to the site identity to help some thing appealing.
ReplyDeleteInitially when i first manifested itself 2 alternative benefits,
although the masai have a improved title. Nevertheless some tips i
required I came across here.
Here is my web page ... How To Get Rid Of Genital Warts