ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 20, 2013

CCM YAUNGURUMA NYAMAGANA LEO: NAPE AJA NA SIRI ZA KIFO CHA CHADEMA

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dr. Antonty Diallo akizungumza na wananchi pamoja na wanachama toka meza kuu leo jijini Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana.


Mbunge wa Kwimba Mh. Mansoor akizungumza leo jijini Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana.


 Mbunge wa Rolya Mh. Lameck Airo akiwa sambamba na mmiliki wa shule ya Aliance Accademy kwenye jukwaa kuu leo jijini Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo (L), Mwenyekiti wa CCM Nyamagana Raphael Shilatu (C) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Anthony Diallo (R) wakipanga mikakati kwenye meza kuu kuhusu yale yanayo endelea kujiri leo jijini Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana.


Kiapo kwa wanachama wapya wa CCM leo jijini Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza na kanda ya ziwa Musukuma (L) akiwa na Mwenyekiti wa CCM Nyamagana Raphael Shilatu. 



KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kisitafute mchawi anayewamaliza nje ya chama chao.

Alisema ubaguzi ulioota mizizi kwa muda mrefu ndio unaokimaliza chama hicho ambao umelelewa na waasisi pamoja na viongozi wa kitaifa hivyo kina haki ya kufa kutokana na dhambi hiyo.


Bw. Nnauye aliyasema hayo leo jijini Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Bw. Philip Mangula, baadhi ya Mawaziri na maelfu ya wananchi wa jiji hilo na vitongoji vyake.

Alisema matatizo yanayokikabili CHADEMA kutokana na dhambi inayofanywa na viongozi wake ambayo Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliikemea na kudai ni sawa na kula nyama za mtu inakipa fursa chama hicho kuandaa mazishi kwani hakina jinsi ya kujinusuru na kifo.

Alidai kushangazwa na viongozi wa CHADEMA kuendelea kukinyooshea kidole chama tawala na kudai kinahusika na migogoro inayoendelea katika chama chao wakati CCM iliwahadharisha mapema juu ya madhara ya ubaguzi.

“Sisi tuliwaeleza mapema kuwa, ubaguzi ambao wanaukumbatia licha ya kuathiri umoja na mshikamano ni dhambi inayoweza kukisambaratisha chama chao.

“Hamuwezi kuwa na chama ambacho kinaendekeza ubaguzi...ili kiongozi wake adumu na kuheshimika, lazima atoke ukanda fulani au ukoo fulani vinginevyo anasukiwa mizengwe na kutimuliwa.

“Walianza na marehemu Chacha Wangwe...hivi sasa wameanza kumuandama Zitto Kabwe (Naibu Katibu Mkuu CHADEMA), na wanaoitwa vijana wake, nasikia wiki ijayo wamejipanga
kumfukuza John Shibuda (Mbunge wa Maswa Magharibi), wiki ijayo,” alisema Bw. Nnauye.

Bw. Nnauye aliongeza kuwa, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema dhambi ya ubaguzi ni kubwa hivyo chama hicho hakina jinsi ya kuachanana na ubaguzi unaoendelea.

Alidai kuwa, kama CHADEMA ambacho ni chama kidogo kinabaguana kiasi hicho, wakipewa dhamana ya kutawala nchi hali itakuwa mbaya zaidi.

“Kama wanabaguana ndani ya kichama kidogo ambacho hakijai hata mkononi, watafanyaje wakipewa dhamana ya kuongoza hata kipande cha nchi yetu? Alihoji Bw. Nnauye na kudai kuwa, ubaguzi ndani ya CHADEMA umejikita kwenye ukanda, ukabila na udini

Alisema ubaguzi huo unajionyesha zaidi kwenye safu ya uongozi wa chama chao na maeneo mengine ndio maana ameamua kuwapa ushauri wa bure ili wasiendelee kumtafuta mchawi nje ya chama.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.