ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, January 20, 2013

WADAU KIBAO WAJITOKEZA KUONA UFUNGUZI MASHINDANO KOMBE LA MATAIFA AFRIKA KUPITIA DStv, KIOTA CHA SAMAKI SAMAKI MLIMANI CITY JIJINI DAR

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania ambao ni wasambazaji wakuu wa Ving'amuzi vya DStv,Salum Salum (kulia) akizungumza na Wapenzi wa soka walikuwa wamefurika kwa wingi kwenye kiota cha Samaki Samaki,Mlimani City jijini Dar es Salaam jioni ya leo kwa kushuhudia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (yanayofanyika huko nchini Afrika ya Kusini),ambapo DStv waliendesha zoezi hilo na pia kuchezesha bahati nasibu kwa wapenzi hao wa Soka walikuwepo hapo.Kushoto ni Meneja Mahusiano wa Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Salum Salum na Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo,Barbara Kambogi wakichezesha droo ya bahati nasibu ya Shinda King'amuzi cha DStv katika kipindi hiki cha Mashindano ya Kombe la Afrika.

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania,Barbara Kambogi (kushoto) akikabidhi King'amuzi hicho kwa Mshindi wa bahati nasibu hiyi,ambaye ni Mwanalibeneke wa Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog,Othman Michuzi (pili kulia) mara baada ya kuibuka kidedea.(Duuhh.....!! jamaa anazali huyu!).


Baadhi ya Wadau wa DStv wakifuatilia Mtanange wa Ufunguzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika,kati ya timu ya Cape Verde na Afrika ya Kusini ambao ulimalizika kwa kutoka suluhu ya bila kufungana.

Wadau kibao toka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar wakiwa kwenye Kiota cha Samaki Samaki jijini Dar kufuatilia Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika uliokuwa ukirushwa moja kwa moja kupitia DStv kutokea nchini Afrika ya Kusini yanakofanyika Mashindano hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.