Wanasiasa wawili wa
Kenya wanaotaraji kugombea uongozi na ambao wameshtakiwa na Mahakama ya Uhalifu
ya Kimataifa, ICC, kwa kuchochea fujo baada ya uchaguzi, wametangaza rasmi kuwa
wanaungana katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Katika mkutano wa
hadhara uliofanywa mjini Nakuru makamo wa Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, alisema
atagombea urais na waziri wa zamani, William Ruto, alisema yeye atakuwa mgombea
mwenza wa Bwana Kenyatta.
Siku ya Ijumaa shirika
la Kenya la kutetea haki (the International Centre for Peace and Conflict)
lilifikisha kesi mahakama makuu kudai kuwa wanasiasa hao hawafai kushika
madaraka.
Wanasiasa wengine
maarufu wa Kenya piya wameshtakiwa na ICC.
Chanzo: BBC Swahili.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.