MBUNGE wa Jimbo la Rorya Bw. Lameck
Airo “La-Kairo” amememshutumu Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Bw. Ezekial Wenje kwa
kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara ambapo Wenje
alidai kuwa alipewa hundi feki na Mbuge Lameck yenye thamani ya shilingi milioni
tano (Tshs.5,000,000/=) ya benki ya Standard Charted kwenye harambee ya
kuchangia madawati ya jimbo la Nyamagana jijini Mwanza.
Akizungumza
ofisini kwake hii leo mbele ya vyombo mbalimbali vya habari Jijini Mwanza Bw.
Airo amesema kuwa amesikitishwa kuona Mbunge huyo kijana kaanza kulewa madaraka
ya uwakilishi na hata kudiliki kusema maneno ya uongo jukwani wakati
akiwahutubia wananchi wa jimbo lake kwenye mikutano yake ya hadhara kwa nia ya
kujiongezea umaarufu wa kisiasa.
Sikiliza alichosema kwa kubofya play..
Sikiliza alichosema kwa kubofya play..
Haya
yanaibuka ikiwa ni takribani miezi sita sasa tangu kutolewa kwa cheki hiyo
ambapo mbunge huyo wa Lorya anahoji kwamba kama Wenje anasema kuwa cheki hiyo
ilibaunsi hivyo ni feki kwanini hakumtafuta kwa njia ya simu kuwasilisha
malalamiko.
Mh.
Lameck ameongezea kwa kudai kuwa hata siku fedha hizo zinatolewa alipigiwa simu
na wadau wa benki kupewa taarifa za uhamishaji wa fedha.
Alipotafutwa
kwa njia ya simu ili kubaini ukweli wa haya yaliyosemwa na Bw.Airo,
Bw.Wenje amekanusha kumtaja mbunge huyo kuwa alimpa hundi feki
sambamba na kukanusha kiasi kinachotajwa kwamba kilitolewa kwamba si shilingi
milioni tano bali ni milioni moja tu ambayo haikuwa na matatizo yoyote kwani
Benki na aliweza kuitoa na kuhamishia katika Akaunti maalum kwa ajili ya kutengenezea
madawati kama ilivyokuwa imekusudiwa.
Sikiliza kilichosemwa na wenje mkutanoni kwa kubofya play..
Sikiliza kilichosemwa na wenje mkutanoni kwa kubofya play..
Mtandao huu uko mbioni kufuatilia stakabadhi za uhamishaji fedha hizo kubaini ukweli.
Katika
hatua nyingine Bw.Airo ameendelea kusisitiza kauli aliyoitoa hivi karibuni kuwa hato gombea Ubunge wa
Jimbo la Rorya baada ya kumalizika uongozi wake wa miaka mitano.
Bw.
Airo aliongeza kuwa CCM Wilaya ya Rorya ina wawakilishi wengi wazuri wa kuongoza na kusimamia ilani za Chama cha Mapinduzi, hivyo haoni sababu za kuhofia wanachama wenzake watakao jitokeza kugombea kuteuliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ugombea ubunge jimbo hilo naye atakuwa mstari wa mbele kupambana na kuhakikisha kuwa anampigia debe mgombea huyo hadi ushindi upatikane.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.