TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NOVEMBA 22, 2012
Masahihisho
ya picha iliyotolewa na gazeti la Uhuru wakati bondia Onesmo Ngowi na David
Migeke wakitia sahihi mkataba baina yao wa kupigana pambano lililofanyika
katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-Es-Salaam ni mwaka 1983 na sio 1987.
Onesmo Ngowi alimdunda David
Migeke kwa KO raundi ya 2 (pili) katika mpambano ulioandaliwa na kampuni ya
Safari Sound Promotions ya jijini Dar-Es-Salaam ambayo ilikuwa inamiliki bendi
ya musiki ya Orchestra Safari Sound chini ya mfanyabiashara maarufu bwana Hugo
Kisima wa jijiniDar-Es-Salaam.
Wafadhili wakuu wa mpambano huo
walikuwa Tanzania Bottlers (Coca Cola), Tanzania Distilleries (Konyagi), Kamin
Industries na Chibuku.
Baada ya mpambano huo ambao
ulikuwa moja ya mapambano mengi ya ushindi kwa Onesmo Ngowi alipata nafasi ya
kugombea mkanda mpya wa Afrika Mashariki na Kati jijini Nairobi Kenya akichuana
na bondia wa Kenya aliyekuwa anapigana ngumi nchini Japan Modest Napunyi Odour,
June 1983. Mpambano huo ndio ulioanzisha ngumi za kulipwa nchini Kenya na
Uganda.
Ngowi alihamia Nairobi, Kenya
Septemba 1983 na kuondoka mwaka mmoja baadaye Decemba 1984 na kuhamia barani
Ulaya katika nchi ya Ugiriki ambako alicheza ngumi chini ya Kampuni ya bingwa
wa mieleka Ulaya George Tromaras (Tromaras Sports Arena) na kustaafu mwaka 1988
akiwa ameshamia nchini Denmark!
Imetumwa na:
Onesmo Ngowi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.