ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 16, 2012

UCHAGUZI MKUTANO MKUU CCM MKOA WA MWANZA NGOMA NZITO NAFASI YA UENYEKITI: NI MABINA AU DIALLO AU...?

Mkutano mkuu wa mkoa wa Mwanza 2012 kupitia CCM unaendelea sasa kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo wajumbe takribani 1015 kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza wanasifa za kushiri uchaguzi huu kumpata Mwenyekiti, Wajumbe mkutano mkuu wa mkoa kwa kila wilaya, Katibu Itikadi na uenezi pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha.


Yote tisa kumi kiu ya wengi wanachama wa CCM na wananchi wa mkoa huu wanasubiri kwa hamu matokeo ya nafasi ya U-enyekiti CCM Mkoa wa Mwanza, kuna wagombea watano ktk nafasi hiyo, na wagombea wanaotajwa na vinywa vya wengi kuitwaa nafasi hiyo ambao ni Diallo na Mabina mbao tangu awali wamekuwa wakipeana vijembe vya chini chini kimtindo. Swali jeh! ni wao au mwingine asiyetarajiwa?
Wajumbe kutoka Ukerewe.


Wajumbe kutoka Nyamagana.


Wajumbe kutoka Sengerema.


Wajumbe kutoka Kwimba.


Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi mkoa wa Mwanza mbunge wa Sengerema Mh. William Ngereja akitoa maelezo juu ya taratibu mbalimbali za mchakatomzima unaoendelea uwanjani hapa akiwa meza kuu na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge Mh. William Lukuvi (katikati) na katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza  Joyce Masunga.


Mwenyekiti wa CCM wilaya Geita Joseph Kashegu aka Musukuma (kushoto) na Mstahiki meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani Shanslaus Mabula. 


WajumbezZZZ mkutanoni ....

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.