Wanausalama barabarabani wakipima ajali hiyo iliyosababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ni dereva wa basi lenye namba za usajili T 853 BRB lililokuwa na wajumbe hao. |
Basi lenye namba za usajili T 853 BRB lililokuwa na wajumbe hao likiwa katikati ya barabara mara baada ya kupata ajali. |
Imetokea ajali ya basi lililobeba wajumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Kwimba, ambapo basi lao limepata ajali na kuanguka eneo la Buhongwa wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza majira ya saa 3:30 - 4:00 asubuhi ambapo inatajwa kuwa dereva wa chombo hicho cha usafiri amefariki dunia papo hapo na wajumbe wengine saba kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali ya rufaa Bugando.
Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa basi hilo lililokuwa katika mwendo kasi lilikuwa katika harakati yakulikwepa roli aina ya fuso ambalo lilikuwa likigeuza kujiweka sawa kuingia barabarani ndipo basi hilo lilipopoteza uelekeo na kulibamiza fuso na kupinduka.
Wajumbe hao kutoka wilaya ya Kwimba, walikuwa wakiingia jijini Mwanza kwenye uchaguzi wa viongozi na wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza unaofanyika leo uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.