Said Mundi (aliye vaa mkanda wa ubingwa). |
Bondia bingwa wa taifa wa kilo 59 toka mkoa wa Tanga Said Mundi "smart punch"amefiwa
na baba yake mzazi mzee Abdulrahman mbaraka nyumbani kwake Zahrau
mkoani Tanga.
Kifo hicho kilitokea jioni ya jana muda mchache kabla ya
mpira wa simba na yanga haujaanza,sababu ya kifo chake cha ghafla
inaelezwa ni shinikizo la damu lilitokea kwa muda mfupi na kujaribu
kumpeleka katika hospital bombo na kufia njiani, kwa maelezo ya said
mundi mwenyewe kwa Ibrahim Kamwe"bigright" ni
kuwa baba yake hapo awali hakuwa na ugonjwa huo umekuja ghafla na
umemchukua baba. Wanategemea kuzika leo jioni.
Said
Mundi anaetegemea kupanda ulingoni tarehe 26 octoba 2012 kuzichapa na
jumanne Mohamed raundi kumi kugombania ubingwa wa PST katika uwanja wa
mkwakwani-Tanga.viongozi wote wa masumbwi kwa pamoja tupo pamoja na said
mundi katika wakati huu mgumu uliompata na tunashirikiana katika
shughuli zima za kufanikisha msiba huu.Mungu ailaze roho ya mzee Abdi
Mbaraka mundi peponi - amin
Taarifa na "big right"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.