ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 2, 2012

AIRTEL YASHEREHEKEA UZINDUZI WA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NA WATEJA WAKE

Meneja Huduma kwa wateja wa Airtel Aneth Muga akitoa ufafanuzi wa moja ya huduma kwa wateja waliotembelea duka la Moroco leo ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja inayoanza leo ambapo Airtel inasherehekea na kuwashukuru wateja wake nchi nzima. Pichani ni baadhi ya watoa huduma kwa wateja wa Airtel wakiwapatia huduma wateja.


Wafanyakazi wa Airtel wakitoa huduma  ya internet kwa a wateja waliotembea katika duka la Airtel lilipo Moroco jijini Dar es saalm ambapo Airtel leo imesheherekea uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja na kuwashukuru wateja wake kwa kutumia huduma na mtandao wa Airtel

Mkuu wa kitengo cha  huduma kwa wateja Adrian Lyamba (katikati) akiwaongeza wafanyakazi na wateja wa Airtel kukata Keki wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja ambapo Airtel imejumuika na wateja wake  katika kusherehekea  na kutaka keki pamoja na kuwashukuru kwa kutumia mtandao wa Airtel

Mkuu wa kitengo cha  huduma kwa wateja Adrian Lyamba akimlisha keki moja ya wateja aliyetembelea katika duka la Airtel lilolopo Moroco jijini Dar es saalam wakatii wa ufunguzi wa wiki ya huduma kwa wateja  ambapo Airtel imefungua wiki ya huduma kwa wateja wiki nzima kwa kusherehekea na kuwashukuru wateja wake nchi nzima.  Halfa hiyo imefanyika katika makao makuu ya Airtel jijiini  Dar es saalam
Mfanyakazi wa huduma kwa wateja Atupiana Msuya  akigawa vinywaji kwa baadhi ya wateja waliohudhuria uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam.

Mmoja wa wateja akimlisha keki  Mkuu wa kitengo cha  huduma kwa wateja Adrian Lyamba wakati wa  uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wa kitengo cha huduma kwa wateja wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es saalam

Mkuu wa kitengo cha  huduma kwa wateja Adrian Lyamba akiwakabidhi wateja walioko kwenye magari vipeperushi vyenye  maelezo kuhusu bidhaa za Airtel wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja uliofanyika leo .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.