ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 21, 2012

TPBC YAIPIGA JEKI BFT


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 19/09/2012


Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) jana imelipiga jeki Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Nchini (BFT) katika mashindano yaliyomalizika katika uwanja wa ndani wa Taifa jana tarehe 19/09/2012.


Rais wa TPBC bwana Onesmo Ngowi alimkabidhi Katibu Mkuu wa BFT bwana Makoye Mashaga zawadi za washindi wa kwanza na wa pili katika mashindano ya ngumi za ridhaa za taifa yaliyoshirikisha mabondia kutoka katika mikoa zaidi ya 19 ya Tanzania bara.


Bwana Ngowi alimweleza katibu Mkuu wa BFT kuwa TPBC inaungana na BFT katika kuendeleza ngumi nchini wakijua wazi kuwa ni katika mashindano kama haya Tanzania inawapata wawakilishi wake katika mashindano ya kimataifa.


Ushirikiano huu wa TPBC ulianza tangu wakati wa Katibu Mkuu wa zamani wa iliyokuwa TABA marehemu Narcis Tarimo.


Akimwelezea zaidi msaada wa TPBC katika mashindano ya taifa, Rais wa TPBC bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa ni ngumi za ridhaa pekee ambazo zinaweza kuleta mwelekeo wa maendeleo ya ngumi nchini.


Ngowi alisema kuwa kama hakuna msingi mzuri wa ngumi za ridhaa ni wazi kuwa hakutakuwa na ngumi nzuri za kulipwa kwani msingi wa ngumi unaanzia kwenye ngumi za ridhaa.


Rais huyo aliyekuwa bondia maarufu wakati wa ngumi za ridhaa na kulipwa miaka ya 80 na 90 kiasi cha lupewa jina la “Piston Mover”(mwendo wa piston ya gari) kwa ajili ya kasi ya mikono na miguu yake alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufundisha ufundi kwa mabondia ili waweze kucheza ngumi za ufundi.


“Kuna tofauti kubwa sana kati ya ngumi za ridhaa na ngumi za kulipwa” aliendelea kusisitiza Rais huyo.


“Wakati mabondia wa ridhaa wanapewa points wakati wanapopiga ngumi za ufundi za kichwani, bondia wa ngumi za kulipwa anatakiwa aweze kumzidi mpinzania wake kwa kila kitu” aliendelea kusisitiza Rais huyo.


Mabondia wetu wa ridhaa wanatakiwa wafundishwe namna ya kupiga ngumi za ufundi kichwani na ziwe nyingi ndipo wanaweza kushinda kwenye mashindano ya kimataifa” alimalizia kusisitiza Ngowi.


Ushirikiano wa TPBC na BFT unaleta sura mpya kwenye tasnia ya ngumi nchini na inaonyesha mwanga mzuri mbele ta safari.


Mgeni rasmi katika fainali za mashindano hayo alikuwa ni Katibu Mkuu wa BMT bwana Henry Lihaya na alimshukuru Ngowi kwa msaada huo wa TPBC.

Aidha, Ngowi alikabidhi baadhi ya zawadi kwa washindi walioshinda katika fainali hizi za mwaka 2012.


Mungu zibariki ngumi Tanzania, Mungu ibariki nchi yetu nzuri Tanzania.


Imetolewa na Uongiozi


Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.