TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makore Mashaga, Katibu BFT Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Juliana Yassoda leo atafunga mapamano ya fainali ya ngumi ya ubingwa wa taifa kwenye uwanja wa ndani wa taifa kuanzia saa tisa alasiri.
Katika fainali hiyo mabingwa wa kila uzani wataiuka na medali za kwanza za dhahabu na kitita cha shilingi 30,000 kila mmoja.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mchezo huo nchini (BFT), Makore Mashaga alisema kwamba michezo 9 ya wanaume na miwili ya wanawake itachezwa kwenye fainali hiyo ambayo itawakutanisha mabondia wa uzani wa chini hadi ule wa juu.
Mashaga alisema bingwa wa kila uzani atajinyakulia medali ya kwanza ya dhahabu na pesa tasilimu Tsh 30,000 kila mmoja huku washindi wa pili wakiondoka na medali ya Fedha na Tsh 20,000 kila mmoja.
"Washindi wa tatu wa kila uzani watapata 10,000 kila mmoja pamoja na medali za Fedha," alisema Mashaga na kufafanua kwamba kwa upande wa medali ya tatu washindi ni mabondia wawili katika kila uzani waliopoteza mapambano yao ya nusu fainali," alisema Mashaga.
Katika mapambano ya juzi, Said Hofu wa JKT alitinga fainali baada ya kumpiga Hafidh Bamtulah, wengine waliongia fainali ni Maulid Athuman Wa Polisi aliyempiga Maro James wa Ruvuma Mabondia wengine waliotinga fainali ni Mathar George wa Kilimanjaro atakayezichapa na Ireny Kimaro wa Tabora kwenye uzani wa light fly wakati Ester Kimbe wa Ngome atatoana jasho na Mariam Nyerere wa Dodoma katika uzani huo.
Kwa wanaume matokeo ya nusu fainali iliyochezwa juzi jioni kati ya Hashim Saimon wa Ngome na Victor Njaiti wa JKT, Badi Mumbamba wa Temeke dhidi ya Seleman Bamtulah wa Magereza, Mohamed Chibumbuli wa Magereza dhidi ya Omar Jongo wa Temeke ndiyo yaliamua washindi watakaocheza fainali ya leo.
Mapambano mengine yalikuwa kati ya Alex Matero wa Temeke dhidi ya Joseph Martin wa JKT, Yusuph Ndimbo wa Mbeya dhidi ya Shaban Ngaoneka wa Ilala, Yahaya Malik dhidi ya Hamad Furahisha.
|
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.