AIRTEL YAPEWA CHETI CHA HESHIMA KWA KUWA WADAU WAZURI USALAMA BARABARANI
Maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani yamefanyika Rasmi mkoani Iringa huku maandamano maalum kwaajili ya kuhamasisha jamii kuzingatia sheria barabarani yakifanyika katika viwanja vya Samora mkoani hapo.
Katika maadhimisho hayo kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ilikabidhiwa cheti cha kushiriki na kuwa wadau wazuri wa usalama Barabarani
Akiongea katika maadhimisho hayo Katibu Mwenezi wa Usalama barabarani Bw, Heri Bantu ameyataka makampuni na taasisi mbalimbali kuiga mfano wa kampuni ya Airtel kwa kutoa mchango wa hali na mali katika kupunguza ajali Barabarani . aidha amewataka wananchi wote kuwa makini kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani,
Mara baada ya kukabidhiwa cheti cha Heshima kwa mchango Airtel Tanzania wamesema wataendelea na kampeni yao ya kuhakikisha ujumbe wa usalama barabarani “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA” unafikia walengwa wote kupitia njia mbalimbali za mawasiliano
“Airtel Tanzania tunaendelea na dhamira yetu ya kuhakikisha Usalama barabarani pamoja na kupunguza vifo vya ndugu zetu kutokana na ajali vinapungua,hivyo tumeanza kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwa wateja wetu nchini kuwasihi kuheshimu sheria barabarani ili kuokoa maisha ya wengine alisema Mmbando Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania
Airtel Tanzania ni wadhamini wa kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa miaka mitano mfululizo sasa na kwa mwaka huu Airtel imejitolea uchapishaji wa stika za usalama barabarani pamoja hilo pia Airtel imeshaweka mabango yenye kutoa tahadhari za barabara kwa abiria na madereva katika barabara mbalimbali zilizopo nchini kwa lengo la Kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.