ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 19, 2012

MBUNGE WA KISESA AKABIDHI VIFAA KWA VITUO VYA AFYA JIMBO LA KISESA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 15.

Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga J. Mpina (kulia) akikabidhi mashuka kwa hospitali ya Wilaya ya Meatu kwa Mkurugenzi wa wilaya hiyo Isaya M. Moses 

Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga J. Mpina (kulia) akikabidhi mashuka kwa hospitali ya Wilaya ya Meatu kwa Mkurugenzi wa wilaya hiyo Isaya M. Moses,  makabidhiano hayo yamefanyika siku ya jumatatu kama sehemu ya ahadi toka kwa mbunge katika kuboresha huduma ya afya jimbo la Kisesa.

Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga J. Mpina (kulia) akikabidhi mashuka kwa kituo cha Afya Mwandoya, kwa Mkurugenzi wa wilaya hiyo Isaya M. Moses,  makabidhiano hayo yamefanyika siku ya jumatatu kama sehemu ya ahadi toka kwa mbunge katika kuboresha huduma ya afya jimbo la Kisesa.

Mbunge wa Jimbo la Kisesa Luhaga J. Mpina (kulia) alikabidhi vifaa vya maabara na madawa vyenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa kituo cha Afya Mwandoya,  makabidhiano hayo yamefanyika siku ya jumatatu kama sehemu ya ahadi toka kwa mbunge katika kuboresha huduma ya afya jimbo la Kisesa.

Sehemu ya vifaa vya maabara na madawa vilivyokabidhiwa na Mh. Mbunge wa jimbo la Kisesa Luhaga J. Mpina kwa vituo vya afya jimboni kwake.

Mkurugenzi wa wilaya hiyo Isaya M. Moses,  kwa niaba ya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Meatu amemshukuru mbunge huyo wa Jimbo la Kisesa kwani ni sehemu ya kuisaidia harakati za maendeleo. Amempongeza kwa kuelekeza nguvu zake kuboresha elimu na sasa ameelekeza nguvu kwenye afya ili kukwamua afya za za wakazi wa wilaya ya Meatu.

Nesi wa kituo cha Afya Mwandoya Aneles Lubaganya akiwa kazini ndani ya kituo chake cha kazi.

Huduma zikiendelea Kituoni cha Afya Mwandoya.

Pamoja na kupokea msaada huo wa mashuka 42, vifaa vya maabara na madawa bado kituo cha Afya cha Mwandoya kinakabiliwa na uhaba wa huduma muhimu ya maji suala linalokwamisha shughuli mbalimbali hususani suala la usafi,   Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Mkuu wa kituo hicho cha Mwandoya Dr. Samson Sulubale (Pichani)

Pamoja na kuhofia juu ya mlipuko wa magonjwa kwa kukosa maji, Hofu nyingine ya Mganga Mkuu wa kituo hicho cha Mwandoya Dr. Samson Sulubale ni kuwa mashuka yote ya msaada waliyokabidhiwa kwa mpango huu wa wa kuendesha kituo bila kupata huduma ya maji safi na salama, kuna kila dalili kuwa mashuka hayo yatafubaa. 

Kwa mujibu wa Mh. Mbunge Luhaga Mpina amesema kuwa upo mpango wa kuboresha huduma za  maji kwa mji wa Mwandoya, suala ambalo limekwisha wasilishwa kwenye wizara husika serikalini.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.