ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 18, 2012

SERIKALI YAJIZATITI KUKUSANYA KODI ZA MAJENGO NCHINI KWA KUJA NA TEKNOLOJIA NA MFUMO MPYA

Washiriki walioshiriki semina ya mafunzo kwa kikosi kazi cha kusimamia kodi za majengo miji mbalimbali kwa mikoa yote hapa nchini ikifanyika kwa muda wa wiki moja hivi karibuni ndani ya Naura Spring Hotel mjini Arusha.

Semina hiyo imesimamiwa na TAMISEMI Kitengo cha TSCP  (Ofisi ya Waziri Mkuu RALG) kwa ushirikiano wa DANIDA imekuja ikiwa na lengo la kusimamia vyema na kufuatilia kikamilifu kodi za majengo nchini ili kuongeza pato la Serikali, kupitia mafunzo hayo wanasemina wamepata fursa kujifunza mifumo mipya ya namna ya kukusanya kodi hususani za majengo.

QA Team walioshiriki mafunzo hayo kutoka mkoa wa Mwanza.

Moja kati ya manufaa ya mafunzo hayo kwa taifa letu ni kuwa mpango huo utaisaidia Serikali katika kufanikisha zoezi la ukusanyaji kodi za majengo kwa ufanisi.

Utaboresha upatikanaji wa  kodi zote bila ukukwepaji.

Utasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri za miji nchini hasa ukizingatia kuwa Halmashauri nyingi nchini fedha zake zimekuwa zikipotea kutokana na uduni wa ukusanyaji.

Jumla ya washiriki 70 kutoka  Halmashauri za miji mbalimbali hapa nchini wamehudhuria Semina hiyo. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.